FUTA MACHOZI

(Makala ya 9 Kati ya 100 mwaka huu 2022)

Machozi Ni ishara inayotafsiri hisia zilizofichika chini kabisa ya uvungu wa moyo wa mtu.

Watu hutoa machozi kwasababu ya maumivu na wengine kwasababu ya furaha. Muktadha na mazingira yatakayokuwepo ndiyo hutuambia watazamaji kuwa machozi yako yanatafsri hisia gani ndani ya moyo wako.

Lakini yote juu ya yote unapaswa kukumbuka kuwa matukio mengi hutokea Mara moja tu, baada ya hapo yaliyobaki huwa Mara nyingi Ni marudio ya tukio ulilolipata, ulilolishuhudia au kulisikia Mara ya kwanza.

Kimsingi zipo nyakati ngumu maishani ambazo hata ukimkuta mtu analia unabaki kusema Ni halali alie kwasababu Ni kweli zinaumiza.

Lakini jambo la msingi ninalotamani tujifunze Ni hili. Kwa kila hatua unayoipitia maishani hasa nyakati ngumu unapaswa kubeba fundisho na sio maumivu.

Fundisho hilo litakusaidia kupita njia itakayokuwa salama zaidi kwa wakati mwingine. Lakini pia litakusaidia kuwaonyesha wengine njia ili nao wasitumbukie shimoni.

Kubeba maumivu Ni kujitwika gunia la misumari kingali una upaa. Lakini utaumia tu. Na kufanya hivyo Ni kujiweka kwenye hatari ya kuipoteza furaha yako ya kweli maishani na kuipokonya Nguvu iliyopaswa kukusaidia kupiga hatua. 

Futa machozi, usiendelee Tena kulia. Angaliaa ulipokwama Kisha angaliaa namna itakufanya uendelee na safari.

   Kumbuka Usisahau; Tough times Never last but tough people do. ✋✋✋
Writer; Jofrey Mwanambesi
Facebook page; Ghala la kumbukumbu
📞📞 0759606160/0623758540


TANGAZA KWENYE APPLICATION YETU KWA GHARAMA NAFUU TUPIGIE 0621663340

No comments