EDWARD NGOYAI LOWASSA AFANYIWA UPASUAJI WA TUMBO

Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Edward Ngoyai Lowassa amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kufanyiwa upasuaji wa tumbo.

Taarifa kutoka kwa familia ya Lowassa zinasema kuwa kiongozi huyo amelazwa katika hospitali hiyo kwa karibu wiki nzima baada ya kufanyiwa upasuaji.

Akizungumza Mbunge wa jimbo la Monduli, Fredrick Lowassa ambaye ni mtoto wa Lowassa amesema baba yake alilazwa katika hospitali hiyo alipopatwa matatizo ya tumbo.

No comments