Hii hapa Siri kubwa kuhusu wanawake
*WANAUME KUNA VITU LAZIMA TUVIELEWE KWA WANAWAKE.*
Biblia inasema: *MWANAMKE NI KIUMBE DHAIFU*
hapo hapo inasema *TUKAE NAO KWA AKILI.*
Na bado inasema *MWANAMKE NI JESHI KUBWA*
Swali?
Walijifunza saa ngapi uwanajeshi na ili kudhibitisha kwamba ni mwanajeshi Mungu anamtuma kwa mwanamme amlinde.
Yeremia 31:22 .... *Kwa maana Bwana ameumba jambo jipya duniani;* *mwanamke atamlinda mwanamume.*
KUMBUKA HILI MWANAUME MWENZANGU.
●Mtu wa kwanza kukutana na SHETANI live ni mwanamke pamoja na kwamba walizungumza mengi na kula tunda kiukweli hatujui mengine waliozungumza mbali na kula tunda.
●MWANAMKE aliumbwa ukiwa usingizini wewe MWANAUME hujui ni kitugani walichozungumza na Mungu kabla ya wewe kuzinduka.
●MWANAMKE ndiye aliyemwelewa Mungu alipoambiwa ana mimba ya Roho Mtakatifu wewe MWANAUME ulitaka kumkimbia badala ya kukabiliana na changamoto hiyo.
●MWANAMKE ndiye mtu wa kwanza kwenda kuhakikisha kama kweli Yesu amefufuka na kusambaza habari.
●MWANAMKE ndiye anayeongoza kwa ushawishi mkubwa mwanaume huna ujanja mfano.
■Eva kwa Adamu
■Delila kwa Samson
■Ester kwa Ahasuero
■Raheli kwa Labani n.k
> *Usimuudhi mke wako ana siri kubwa sana usione kakaa na wewe anakuvumilia pamoja na ukatili wako.*
> *Anaweza akatekeleza walichozungumza na Mungu au anaweza kutekeleza alichozungumza na shetani*
Post a Comment