AMKA NA BWANA LEO 06/12/2021

*KUTOA KILA TUNAPOPATA.*
Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi. *Malaki 3:10.* 

▶️ Mwisho unakaribia haraka sana na watu wengi katika makanisa yetu wamelala usingizi. Hebu wote sasa waifanye kazi ya Mungu kuwa shughuli yao. Mungu amewaaminia watu Wake talanta za fedha, wengine nyingi, wengine kidogo, kuliko wengine. Kwa wengi umilikaji wa mali ni mtego. Katika shauku yao ya kufuata mitindo ya kilimwengu, wamepoteza juhudi yao kwa ajili ya ukweli, na wapo katika hatari ya kupoteza uzima wa milele. Kwa uwiano sawa na jinsi Mungu alivyowafanikisha, watu wanapaswa kurudisha Kwake sehemu ya mali ambayo Mungu ameiweka katika uwakili wao.....

▶️ Hebu wote wachunguze mahusiano yao ya kibiashara na Muumbaji wao kwa uangalifu. Wale ambao hawatasita kumdanganya Muumbaji wao kwa hakika hawatasita kumdanganya mwanadamu mwenzao.

▶️ Ninatamani, kulikazia jambo hili kwa watu kuwa Mungu anawachukulia tendo la kuzuia zaka na sadaka kama unyang'anyaji. Sisi ni mawakili tu wa Mungu; hatumiliki fedha inayopita katika mikono yetu. Katika matumizi ya fedha inatupasa kuwa watendakazi pamoja na Yesu Kristo.

▶️ Inatupasa kuhisi shauku kubwa kwa ajili ya kupanua kazi ya Mungu. Kazi hii imeshakua kwa kiwango kikubwa, lakini inapasa kupanuliwa kwa kasi zaidi. Tunahitaji watendakazi wengi zaidi, na lazima kuwepo roho ya kujikana nafsi kwa watu wote, ili kwa kujenga miundombinu ya kupelekea ujumbe katika maeneo mapya. Katika maeneo mengi kazi imedumaa kwa kukosa fedha. Kemeo la Mungu linawakalia wale wasiojitokeza kutoa msaada Kwake... 

▶️ Katika kazi kubwa ya kuuonya ulimwengu, wale walio na ukweli katika mioyo yao na wametakaswa kwa njia ya ukweli, watafanya sehemu ya kazi waliyopangiwa. Watakuwa waaminifu katika kulipa zaka na sadaka. Kila mshiriki wa kanisa anafungwa kwa uhusiano wa agano na Mungu kujinyima kila matumizi ya fedha yasiyokuwa ya lazima. Hebu mapungufu katika udhibiti wa mapato katika maisha ya nyumbani isiwe sababu ya kutoweza kufanya sehemu yetu katika kuimarisha kazi tayari imeshaanzishwa na kushindwa kuingia katika maeneo mapya.*
*MUNGU AKUBARIKI SANA.*

No comments