AMKA NA BWANA LEO 28/11/2021
JUMAPILI, NOV 28 2021
*ROHO MTAKATIFU — ZAWADI KUU*
_Tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba. Wafilipi 2:8._
📚 Kuinuliwa kwa Kristo kuna uwiano sawa na kudharauliwa na kuteswa Kwake. Alifanyika Mwokozi na Mkombozi, kwa Yeye kwanza kufanyika Kafara. Siri kubwa kiasi gani imo katika utauwa wa Kristo. Baada ya kuithibitisha sheria na kuifanya iheshimike kwa kuyakubali masharti ya kuuokoa ulimwengu kutoka katika uharibifu, Kristo aliharakisha kwenda mbinguni ili kukamilisha kazi Yake, na kutimiza utume Wake kwa kumtuma Roho Mtakatifu kwa wanafunzi Wake. Kwa njia hiyo aliweza kuwahakikishia waumini kuwa hakuwasahau, ingawa sasa akiwa mbele za Mungu, mahali palipo na ukamilifu wa furaha milele zote.
📚 Roho Mtakatifu alipaswa kushuka juu ya wale waliompenda Kristo katika ulimwengu huu. Kwa njia hii wangeweza kupewa sifa, katika na kwa njia ya kumtukuza Kiongozi wao, kupokea kila karama muhimu kwa ajili ya kutimiza utume wao. Mtoa uzima alishika katika mikono Yake, siyo tu funguo za mauti, bali pia mbingu yote yenye mibaraka tele. Alipewa mamlaka yote mbinguni na duniani, na baada ya kukaa katika mahali Pake katika ikulu ya mbinguni, angeweza kuwapa mibaraka hii watu wote wanaompokea.
📚 Kristo aliwaambia wanafunzi Wake, "Yawafaa ninyi mimi niondoke, kwa maana mimi nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu" (Yohana 16:7). Hii ilikuwa zawadi kubwa kuliko zote. Roho Mtakatifu alitumwa kama hazina yenye thamani kubwa kuliko zawadi zote ambazo mwanadamu anaweza kuzipokea. Kanisa lilibatizwa katika nguvu za Roho. Wanafunzi waliwezeshwa kwenda kumtangaza Kristo, kwanza Yerusalemu, mahali ambapo kazi ya aibu ya kumdharau Mfalme Mwenye haki zote za kutawala ilipofanyikia, na ndipo angetangazwa mpaka mwisho wa dunia....
🔘 *Mibaraka inayomiminwa kwa wote wanaomjia Mungu katika jina la Mwanawe ni kamili na ni bure. Ikiwa watazingatia masharti yaliyowekwa katika Neno Lake, atawafunulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagia baraka hata isiwepo nafasi ya kutosha ya kuipokea… Ikiwa watu wa Mungu watajitakasa kwa kuzitii kanuni Zake, Bwana atatenda kazi miongoni mwao. Ataumba upya roho zilizopondeka, zenye unyenyekevu, na kufanya tabia zao ziwe safi na takatifu.*
*MUNGU AKUBARIKI SANA*
Post a Comment