AMKA NA BWANA LEO 18/10/2021

*KESHA LA ASUBUHI*

*_LEO NA MUNGU - Jumatatu, Oktoba 18, 2021_*

*YATAFAKARINI HAYA*

*_Kwa kuwa Bwana anaijua njia ya wenye haki, Bali njia ya wasio haki itapotea. Zaburi 1:6._*

✍🏿 Ikiwa akili imeelimishwa kutafakari mambo ya kimbingu, shauku Ihawezi kutoshelezwa kwa mambo ambayo ni sahili na ya kawaida. Tunapaswa kuzingatia moyoni kwamba Bwana amejiandaa kufanya mambo makubwa kwa ajili yetu, lakini ni lazima tujiandae kuyapokea mambo haya kwa kuondoa kutoka moyoni kujitosheleza na kujiamini kote. Bwana peke yake anastahili kutukuzwa. "Wao wanaoniheshimu," Anasema, "Nitawaheshimu" (1 Samweli 2:30). Hatupaswi kujiweka kwenye adha ya kupenda kutambuliwa, kwani "Bwana anawajua walio wake." Wale ambao hawajitumainii wenyewe, lakini pia kutozitumainia kazi zao wenyewe, ndio ambao kwao Bwana atadhihirisha utukufu wake. Watazitumia vizuri sana baraka walizozipokea. Wale wote wanywao katika vijito safi vya Lebanoni, watakuwa na maji ya uzima yakibubujika ndani yao na haya hayawezi kukomeshwa....

✍🏿 Bwana anajua kwamba kama tukimtumainia mwanadamu, na kumwamini mwanadamu, tunakua tukiutegemea mkono wa kimwili. Anataka tumwendee kwa ujasiri. Hakuna ukomo katika Uweza wake. Mtafakari Bwana Yesu, na wema wake, na upendo wake, na usitafute kuona mapungufu na kuyakalia makosa ambayo wengine wameyafanya. Ruhusu akilini mwako yale mambo ambayo yanastahili utambuzi wako na kusifu kwako; na kama wewe ni mwepesi wa kutambua makosa kwa wengine, hebu uwe mwepesi zaidi kuyatambua mambo mema na sifa njema. Unaweza, kama ukijikosoa, kuona vitu visivyofaa kama vile uvionavyo kwa wengine. Hivyo basi hebu na tufanye kazi kila wakati tukiimarishana katika Imani takatifu.

🔘 *Katika waraka wa Paulo kwa Wafilipi, anasema, "Paulo na Timotheo, watumwa wa kristo Yesu, walioko Filipi, pamoja na maaskofu na mashemasi. Neema na iwe kwenu na amani zitokazo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana wetu Yesu Kristo. Namshukuru Mungu wangu kila niwakumbukapo, sikuzote kila niwaombeapo ninyi nyote nikisema sala zangu kwa furaha, kwa sababu ya ushirika wenu katika kuieneza Injili, tangu siku ile ya kwanza hata leo hivi; nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu" (Wafilipi 1:1-6).*

*MWENYEZI MUNGU AKUBARIKI SANA*

No comments