AMKA NA BWANA LEO 14/10/2021

*KESHA LA ASUBUHI*

*_LEO NA MUNGU - Alhamisi, Oktoba 14, 2021_*

*HUKUMU INAKUJA*

*_Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au likiwa baya. Mhubiri 12:14._*

*✍🏼 Bwana anakuja hivi karibuni katika mawingu ya mbinguni, kwa nguvu na utukufu mwingi. Je! Hakuna uelewa wa kutosha katika maandiko unaolihusu tukio hili, na maandalizi muhimu kwa hilo kutufanya tufikirie kwa uzito wajibu wetu?*

👉🏽 Mada hii inapaswa kuwekwa mbele ya watu kwa upana na kwa uwazi. *_"Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake .... na mataifa yote yatakusanyika mbele zake"_ (Mathayo 25:31,32).*

✍🏼 Wasilisha ukweli unaohitajika kwa kila kanisa kama namna ya kuufikia mwisho, na ambao unamaliza hukumu, na maamuzi na tuzo zake za milele. 

*👉🏽💜Mungu atamlipa kila mtu kulingana na matendo yake. _"Na Henoko mtu wa saba baada ya Adamu, alitoa maneno ya unabii juu ya hao, akisema, angalia, Bwana alikuja na watakatifu wake maelfu maelfu, ili afanye hukumu juu ya watu wote"_ (Yuda 1:14,15).*

*👉🏽 Na Sulemani, alipokuwa akitoa wito wake, na akitangaza kama mhubiri wa haki, aliwakilisha matarajio ya hukumu ijayo. _"Hii ndiyo jumla ya maneno, yote yamekwisha sikiwa," alisema, "Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu. Kwa maana, Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au baya"_ (Mhubiri 12:13,14).*

*✍🏼 Tunao mzigo mkubwa, wa kutangaza ujumbe mzito kutoka katika Neno la Mungu bila Kuruhusu akili zetu kubuni na kupanga kuwasilisha nadharia za watu zisizo na maana kwa kundi la Mungu kama Ukweli ujaribuo. Ambao ni makapi katika ngano.*

*🔘 Hukumu ya mwisho ni tukio kubwa na la kutisha. Hili lazima litokee katika ulimwengu. Baba amekabidhi hukumu yote kwa Bwana Yesu. Ataitangaza thawabu ya uaminifu kwa sheria ya Yehova. Mungu ataheshimiwa na serikali yake kuthibitishwa na kutukuzwa, kwa uwepo wa wakazi wa malimwengu ambayo hayakuanguka. Katika kiwango kikubwa iwezekanavyo serikali ya Mungu itathibitishwa na kuheshimiwa. Hii sio hukumu ya mtu mmoja, au ya taifa moja, bali ya ulimwengu mzima. Haya, ni mabadiliko ya pekee sana yatakayofanywa katika uelewa wa viumbe vyote. Ndipo wote watakapoona thamani ya uzima wa milele.*
*MUNGU AKUBARIKI SANA*

No comments