UMMY; WEKEZENI UJENZI WA MIUNDOMBINU WA MADARASA
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu amewaomba wadau mbalimbali nchini kuhakikisha wanawekeza katika sekta ya Elimu kwa kujenga miundombinu ya madarasa ili kupunguza uhaba wa madarasa nchini.
Akiongea katika Maadhimisho ya miaka 40 ya shirika lisilo la kiserikali Word Vision Tanzania yaliyofanyika kitaifa leo Mkoani Dodoma katika Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa Jijini Dodoma Waziri Ummy amesema kuwa elimu ni kipaombele cha Serikali lakini bado kuna upungufu wa madarasa katika shule zetu za Msingi na Sekondari, upungufu wa waalimu na madawati.
Amesema kuwa takwimu zinaonesha kuwa katika mwaka 2021 wanafunzi wa darasa la saba ni 1,129,129, ambapo mwaka jana ufaulu ulikuwa 82.6 na Serikali inategemea mwaka 2022 ufaulu utaongezeka hadi 83.6 hivyo wanafunzi takribani 944, 855 wanatarajiwa kufaulu na kuanza Kidato cha Kwanza Januari, 2022.
Ameendelea kusema kuwa changamoto iliopo ni kuwa wanafunzi wanaotegemea kumaliza Kidato cha Nne mwaka 2021 ni 422,409 hivyo kuna ongezeko la wanafunzi 522,446 ambao hawatakuwa na vyumba vya madarasa.
Aidha kutoka katika Tozo ya miamala ya mawasiliano tutapokea Shilingi Bil 7 ambazo zitakwenda kujengwa vyumba vya madarasa 560 lakini pia bado tutahitaji vyumba zaidi kwa ajili ya watoto wetu ni vyema wadau wakawekeza katika eneo hilo ili kuunga mkono juhudi za Serikali katika kutoa elimu bora.
Amewataka wadau kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuhakikisha inaboresha miundombinu ya Elimu nchini hasa kwenye ujenzi wa madarasa ya shile za Sekondari kwa lengo la kuhakikisha wanafunzi wanaomaliza darasa la saba na kuwa na sifa wanajiunga na kidato cha kwanza.
Aidha, Amewataka Wakuu wa Mikoa wote nchini kuhakikisha wanajenga madarasa hayo kwa wakati na kuacha kujenga kwa kuzima moto kusubiri hadi mwisho wa mwaka ndipo kuanza kujenga kwa kuwa idadi ya wanafunzi wanaotegemewa kuanza Kidato cha Kwanza inajulikana hivyo wajiandae mapema.
Aidha amesema kuwa kwa mwaka 2022 hakutakuwa na uchaguzi wa wanafunzi awamu ya pili (Second Selection) kwa kuwa Serikali inataka kuona watoto wote wanaofaulu

Post a Comment