PROF. ABEL MAKUBI AKUTANA NA BALOZI WA ITALIA
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi amekutana na kufanya mazungumzo na balozi wa Italia nchini Bw. Marco Lombardi akiwa ameambatana na timu ya wataalam katika ofisi ndogo za wizara jijini Dar Es Salaam.
Pamoja na mambo mengine, mazungumzo hayo yalijikita katika kuona namna ambayo Serikali za nchi zote mbili zinavyoweza kushirikiana na kuweka mpango ambao katika kuboresha sekta ya afya ikiwemo huduma za mama na mtoto, vijana, kubadilishana utaalamu, kuhusisha jamii katika kukabiliana na magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza, upatikanaji wa vifaa katika vituo vya afya pamoja na kusapoti rufaa kwa wagonjwa.
Prof. Makubi amesema mpango huo umetengewa dola Milioni 1.5 ambao utashirikisha nchi za Kenya na Uganda na utaanza kufanyiwa kazi mara baada ya wataalamu kukaa na kujadili kwa pamoja kuona namna gani utaweza kutekelezwa nchini.
Kwa upande wake Balozi Marco ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuonesha ushirikiano mkubwa na nchi yake na kuahidi kuendelea kushirikiana katika kuboresha sekta tofauti nchini lengo likiwa ni kupambana na umaskini na kuwawezesha wananchi kuwa na afya bora.

Post a Comment