MR. ARIEL HENRY AMTUMBUA KIGOGO MWINGINE

Waziri Mkuu wa Haiti, Ariel Henry, ametengua uteuzi wa aliyekuwa Waziri wa Katiba, Rockfeller Vincent, na hatua hiyo inatanguliwa na ile ya ‘kumtumbua’ Mwendesha Mashitaka Mkuu nchini humo.

Mwendesha Mashitaka Bed-Ford Claude alipoteza kibarua chake baada ya kutaka Waziri Mkuu huyo achunguzwe kwa mauaji ya aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Jovenel Moise, ambaye aliuawa miezi miwili iliyopita akiwa nyumbani kwake.

Henry, ambaye aliteuliwa na Rais Moise miezi michache kabla ya kuuawa, anaungwa mkono na jumuhiya za kimataifa lakini baadhi ya wanasiasa wa ndani ya Haiti wameonekana kutokuwa upande wake.

Mtanziko wa kisiasa huo unakuja huku asilimia kubwa ya raia wa Kisiwa hicho wakiendelea kuburuzwa na hali mbaya ya kiuchumi, achilia mbali athari za tetemeko la ardhi lililoua watu zaidi ya 2,200.

No comments