MAJALIWA ATOA MWEZI 1 KWA VIONGOZI WA MIKOA, HALMASHAURI
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewapa muda wa mwezi mmoja viongozi wa mikoa na halmashauri wawe wamekutana na wafanyabiashara wadogo maarufu kama Wamachinga na kupanga namna bora ya usimamizi wa shughuli za biashara ikiwemo kutenga maeneo ya kufanyia biashara zao.
Hatua hiyo ni utekelezaji wa maelekezo ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa jana wakati akizindua mpango wa uelimishaji na uhamasishaji wa sensa ya watu na makazi wa 2022, ambapo aliwataka Wakuu wa Mikoa wawe makini katika zoezi la kuwapanga Wamachinga nchini na kuepuka vurugu, fujo na uonevu.
Ametoa kauli hiyo (Jumatano, Septemba 15, 2021) wakati akizungumza kwa njia ya video na Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu, Naibu Katibu wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Waziri wa Viwanda na Biashara, Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Uongozi wa Wamachinga.
Waziri Mkuu amewaelekeza viongozi wa Halmashauri za Majiji, Manispaa, Miji na wilaya waone namna ya kutumia baadhi ya barabara za katikati ya majiji na miji kufungwa muda wa alasiri ili kuruhusu Wamachinga kufanya biashara zao katika barabara hizo.
“Hii ni fursa nzuri kwa wajasiriamali wetu kufanya shughuli zao," amesema Majaliwa.

Post a Comment