JINSI YA KUZILINDA NDOTO ZAKO
*JINSI YA KUZILINDA NDOTO ZAKO.*
Sehemu ya saba..
*3.Kuepuka udanganyifu wa shetani*
Moja kati ya silaha anayoitumia shetani ili kukwamisha ndoto za watu ni UONGO..
*✔Mtu anapoukubali udanganyifu wa shetani ndani ya moyo wake uwe na uhakika hawezi kufika kwenye hatima yake aliyokusudiwa na Mungu kirahisi, kwahiyo kama una ndoto moyoni mwako hakikisha umeushinda uongo au udanganyifu mbalimbali wa shetani..*
🔶KILICHOUA NDOTO YA ADAMU NA EVA YA KUISHI NDANI YA EDENI MILELE HUKU WAKIFURAHIA BARAKA ZA MUNGU NI UDANGANYIFU WA SHETANI ULIOINGIA NDANI YA MIOYO YAO, NA HUU NDIO UDANGANYIFU ULIOWAKOSESHA ADAMU NA EVA👇..
*👉Mwanzo 3:5 kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, NANYI MTAKUWA KAMA MUNGU, mkijua mema na mabaya.*
✔Sasa nisikilize vizuri mpendwa, shetani aliyewakosesha Adamu na Eva kwa udanganyifu wake hajabadilika, hata wewe anaweza akakukosesha kwa udanganyifu wake ili usiishi kwenye kusudi la Mungu hapa duniani..
*✔Kwahiyo shetani akikudanganya na ukaukubali uongo wake kwenye moyo wako uwe na uhakika atakuwa amefanikiwa kuziua kabisa ndoto zako..*
⛔MIFANO YA UDANGANYIFU WA SHETANI.
*1️⃣ Kukuaminisha kwenye moyo wako yakwamba umeshachelewa kuzifanikisha ndoto zako..*
Moja ya uongo wa shetani ni kukuaminisha kwenye moyo wako yakwamba UMESHACHELEWA kuzifanikisha ndoto zako, hivyo kuendelea kuzing'ang'ania ndoto zako ni kujipotezea mda tu, 👈matokeo ya kuukubali uongo huu wa adui ni👇
*(i) kukata tamaa ya kuomba..*
*(ii) imani yako kwa Mungu kutoweka kabisa..*
*(iii) kuamini yakwamba hautafanikiwa tena..*
👆🏻Ukishafika katika kiwango hiki matokeo yake nikwamba kama haujaolewa utajiona hautaolewa tena, kama haujazaa utajiona hautazaa tena, kama una magonjwa utajiona hautapona tena, kama umetafuta ajira kwa mda mrefu bila mafanikio utajiona hautaweza kupata ajira tena n.k
✔NISIKILIZE MPENDWA, MUNGU WAKO HAJASHINDWA KUKUFANIKISHA HIZO NDOTO ZAKO KWAHIYO USIKUBALI ADUI AKUDANGANYE YAKWAMBA UMECHELEWA, NENO LA MUNGU LINATUTIA MOYO HIVI👇
*👉Habakuki 2:3 Maana njozi hii bado ni kwa wakati ulioamriwa, inafanya haraka ili kuufikilia mwisho wake, wala haitasema uongo; ijapokawia, ingojee; kwa kuwa haina budi kuja, haitakawia.*
👆Kwahiyo shikilia ndoto zako usiziachie, Mungu atakufanikisha USIOGOPE..
*2️⃣Adui anaweza kukuaminisha yakwamba Mungu wako amenyamanza kimya*
Uongo mwingine wa shetani ni kukuaminisha yakwamba Mungu wako amenyamanza kimya, maombi yako unayoomba hayafiki mbele za Mungu, kwahiyo kutegemea maombi ili ufike kwenye hatima yako ni kujipotezea mda tu..
🔶NISIKILIZE VIZURI MPENDWA, MUNGU WAKO HAJANYAMANZA KIMYA, YUPO PAMOJA NA WEWE KUHAKIKISHA UNAIPATA HAKI YAKO
*👉Isaya 62:1 Kwa ajili ya Sayuni sitanyamaza, na kwa ajili ya Yerusalemu sitatulia, hata haki yake itakapotokea kama mwangaza, na wokovu wake kama taa iwakayo.*
🔶Ni hivi, kwakuwa wewe ni mwenye haki Mungu hawezi kuyakataa maombi yako..
*👉Zaburi 66:20 Na ahimidiwe Mungu asiyeyakataa maombi yangu, Wala kuniondolea fadhili zake.*
✔Kwahiyo adui kukupa mawazo ya kukukatisha tamaa yakwamba maombi yako hayafiki mbele za Mungu huo ni udanganyifu ili usiendelee kuomba kisha usifike kwenye hatima yako njema aliyokukusudia Mungu👈 HIVYO USIKUBALI UONGO HUU KWA JINA LA YESU..
*✔Narudia tena, Maombi yako hayapotei, machozi😢 yako unayotoa mbele za Mungu kila siku hayadondoki bure, yapo kwenye madhabahu ya Mungu, endelea kuomba WALA USIKATE TAMAA KWA MAANA UTAVUNA KWA WAKATI WAKE USIPOVUNJIKA MOYO..*
⛔Kwahiyo kama unataka kufika kwenye ndoto zako hakikisha umeushinda udanganyifu wa shetani ndani ya moyo wako kwa jina la Yesu..
🔶MWISHO..
*👉2 Kor 11:3 Lakini nachelea; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikira zenu, mkauacha unyofu na usafi kwa Kristo.*
Mungu wa mbinguni awabariki sana🙏
WhatsApp +255657117595
Mwl.Joseph Leonard
Post a Comment