AMKA NA BWANA LEO 3/09/2021

*KESHA LA ASUBUHI.*

Ijumaa, 03/09/2021

*KUFADHILIWA ZAIDI YA MALAIKA.*

*Bwana, kama wewe ungehesabu maovu, Ee Bwana, nani angesimama? Lakini kwako kuna msamaha, ili Wewe uogopwe.* Zaburi 130:3, 4

▶️ Kwa wale ambao wamefanya njia za kigeni kwa ajili ya miguu yao, Bwana huwapa maneno ya kutia moyo. Atakubali maombi yao, ikiwa watatubu na kuongoka. Kupitia kafara isiyo na kikomo ya Kristo, na kwa imani katika jina Lake, wanaweza kupokea ahadi za Mungu. Wana wa Adamu wanaweza kuwa wana wa Mungu. Ni jinsi gani tunapaswa kujazwa na shukurani kwamba kwa kitendo cha Kristo kuchukua ubinadamu, watu walioanguka wamepewa jaribio la pili Kristo anawaweka mahali panapofaa. Kupitia muunganiko pamoja naye wanaweza kuwa watendakazi pamoja na Mungu. Kupitia neema inayotolewa kila siku na Kristo, wanaweza kuinuliwa na kukuzwa kuwa wana na binti za Mungu. Upendo kama huo hauna kifani. 
 
▶️ Yesu anataka utii mkamilifu. Lazima kuwe na kazi kamilifu, ya kiutendaji. Kila siku tunapaswa kuongezeka katika maarifa ya kuyajua mapenzi ya Mungu. Kristo atatoa Roho wake kwa wote ambao kwa umoja watafanya kazi kwa unyenyekevu. 
 
▶️ “Ninyi si mali yenu wenyewe; maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu, na kwa roho zenu, ambazo ni za Mungu” – (1Wakorintho 6:19, 20 KJV). Bei kubwa kiasi gani ililipwa ili kuikomboa jamii ya wanadamu iliyoanguka! Je Haifai kila mtu kuingia katika utumishi wa Mungu, akijitahidi kuboresha talanta alizokabidhiwa, ili zirudishwe kwa Mungu zikiwa pamoja na riba?
 
▶️“Njoni kwangu,” Yesu anasema, “ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo: na (kwa kujifunza na kutekeleza masomo haya) mtapata raha nafsini mwenu” (Mathayo 11:28, 29). Ikiwa tunataka kuishi maisha ya Kikristo, ni lazima daima tushirikiane na Mungu, tukiiacha nafsi kwa kumtegemea Yesu Kristo. Kila siku tunapaswa kufanya kazi kwa ajili ya umilele. 
 
▶️Mwanadamu aliumbwa chini kidogo kuliko malaika. Lakini pale atakapotakaswa na kuhamishiwa kwenda katika nyua za Mbinguni, atakuwa na upendeleo hata kuliko Malaika. 
 
▶️ *Kinachotakiwa kwa ndugu na dada zako, kinachotakiwa kwa yeyote kati yetu ni kuishi maisha ya Kikristo, ya unyenyekevu, tukidhihirisha kwa tabia nguvu iliyopokelewa kutoka kwa Yesu Kristo kupitia muungano pamoja naye.*

*MUNGU ATUBARIKI SOTE.*
🙏🙏🙏🙏

No comments