RAIS MWINYI AFANYA UTEUZI WA MA CEO, MAKATIBU
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi amefanya Uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi, Wakurugenzi mbali mbali na Katibu wa
Kamisheni ya Utumishi kama ifuatavyo;-
1. Kanali Mstaafu Said Ali Hamad ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Ulinzi wa JKU.
2. Ndugu Siyajabu Suleiman Pandu ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Uratibu wa Shughuli za Serikali katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais.
3. Ndugu Khalid Bakar Hamran ameteuliwa kuwa Mratibu Mkuu wa Afisi ya Uratibu wa Shughuli za SMZ - Dodoma Katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais.
4. Ndugu Khamis Haji Juma ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Uendeshaji na Utumishi katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais.
5. Ndugu Khatib Suleiman Khatib ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Nyaraka na kumbukumbu.
6. Ndugu Kubingwa Mashaka Simba ameteuliwa kuwa Katibu wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma.
Aidha, Mheshimiwa Rais amemteua Ndugu Abdul Mohamed (VAN) kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano - Ikulu kuanzia tarehe 23 Julai, 2021.
Post a Comment