KENYA NA TANZANIA ZAJADILI CHANGAMOTO YA COVID-19
Wataalam wa Wizara hizo kutoka nchini Tanzania na Kenya wamekutana jana jijini Nairobi na kuweza kujadili changamoto zinazowakabili nchi hizo mbili ikiwemo ya UVIKO-19 kwa upande wa mipakani.
Prof. Abel Makubi Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto nchini Tanzania amesema mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa Wizara ya Afya jijini Nairobi ulikuwa na lengo la kutekeleza makubaliano yaliyofanyika kati ya Marais wa nchi hizo mbili walipokutana mwaka huu jijini hapa wa kuondoa changamoto za masuala ya Corona kwa upande wa kibiashara.
Amesema mkutano huo ambao ulitanguliwa na kikao cha awali cha wataalum wa sekta hiyo na baadae kufuatiwa na kikao cha Makatibu Wakuu hao waliweza kujadiliana masuala ya upimaji wa Corona baina ya nchi hizo mbili na kuweza kukubaliana ni namna gani ya kuondoa changamoto za ugonjwa huo.
"Tumekutana ili kuweza kuondoa changamoto za Corona ambazo Marais wetu Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan na Mhe. Uhuru Kenyata walikutana na kuona yapo masuala yanayoleta changamoto hususan kwenye biashara kati ya Tanzania na Kenya na kuondoa mashirikiano katika mipaka yetu,hivyo kama wataalam tumekutana ili kuweza kuziondoa changamoto hizo na kuboresha mashirikiano”.
Prof. Makubi alitaja mambo waliyoyajadili ni pamoja na suala la kuhakikisha kwamba kunakuwa na mifumo inayoweza kuwasiliana katika upimaji kwa kuweza kuonekana kwa upande wa Tanzani na wakati huo huo kwa upande wa Kenya.
"Mfano kama mtu amepimwa ‘PCR’ basi aweze kusomwa na kuonekana pande zote mbili na mifumo yetu iweze kusoma kote na hiyo itaweza kusaidia kama nchi na wananchi wetu kuweza kufanya biashara vizuri” Aliongeza.
Aidha, kwa upande wa gharama za upimaji hususan kwa madereva wa magari makubwa alisema wamejadili na kutoa mapendekezo ambayo yatapekekwa kwenye kikao cha Mawaziri wa nchi hizo mbili, kikao ambacho kitakachofanyika siku ya Alhamisi na kuweza kutoa maamuzi ya mwisho.
Kwa upande wa mashirikiano katika kukabiliana na Corona kwa ujumla Prof. Makubi alisema wameweza kujadili masuala ya takwimu,chanjo pamoja na kubadi
Post a Comment