DKT. MOLLEL AMPIGA ZA USO GWAJIMA, IKUBARI CHANJO
1.Kujua mistari yenyewe
2. Kuwa na elimu sahihi ya “Theolojia” ili kujua msingi kwanini mitume au manabii wakasema hivyo pamoja na mazingira.
3. NGUVU ZA ROHO MTAKATIFU (hili ndio la msingi zaidi): hii inakupa ukweli usio andikika kuhusu UFUKIZO wa neno la Mungu
NB: Ukiwa na 1,2 bila 3 huwezi kujua maandiko na kweli ya maandiko na siri za maandiko ya Mwenyezi Mungu.
Linapokuja suala la chanjo siyo suala la yeye kujua kuna DNA , mRNA au live attenuated au jambo lolote, hapo suala je…?
Unamsingi wa sayansi ngumu isiyoshikika na isiyo onekana kwa macho ya kawaida ya vimelea na mwili wa mwanadamu?
Je unajua ili DNA au mnachoita UTU ili uitwe umeguswa maanake nini?
Je, nini kinafanya iguswe…?
Je, kinachofanya paguswe inamausiano yoyote na component za chanjo?
Je, Chanjo ni nini? na ikiingia ndani ya seli inafanya nini? Hayo huwezi kuyajua kwa kina kwenye mitandao au toka kwa marafiki zako wataalamu wa tiba.
Haya upatikana toka kwenye maabara zenye supercomputing systems na zenye watu wachache Duniani wenye uwezo wa kipekee.
Kuhusu chanjo kutumika kuweka watu vifaa, kimsingi ajue tu “Nanotechnology” Nano ni kitu sawa na kusema unachukua sentimita moja unagawa kwa bilioni moja, hivyo ni kitu kidogo sana na hauitaji kutumia chanjo hii kuwekea watu, hata dawa zote tutumiazo ingewekwa pia.
Haya upatikana toka kwenye maabara zenye supercomputing systems na zenye watu wachache Duniani wenye uwezo wa kipekee.
Kuhusu chanjo kutumika kuweka watu vifaa, kimsingi ajue tu “Nanotechnology” Nano ni kitu sawa na kusema unachukua sentimita moja unagawa kwa bilioni moja, hivyo ni kitu kidogo sana na hauitaji kutumia chanjo hii kuwekea watu, hata dawa zote tutumiazo ingewekwa pia.
Tukiwa Bungeni
Mhe. GWAJIMA aliyonyesha wasiwasi huu huu na tulimjibu kuwa maswali yake kuhusu usalama siyo mapya, ndio maswali wanasayansi wetu wanatumia kama hadidu rejea katika kujiridhisha usalama wa chanjo kabla ya kukubali.
NANUKUU
Tukamkumbusha kuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati. Dkt. John Pombe Magufuli alisema tusichukue chochote bila kujiridhisha, ndio maana Rais wetu Mhe SAMIA SULUHU HASSAN ameunda kamati ili kujiridhisha na kila kitu.
Pia tukasisitiza kuwa wanaodhani Tanzania inakataana na ulimwengu au shirika la afya Duniani siyo kweli UBISHI Ni kati ya wanasayansi wa Tanzania na wenzao kuhusu usalama hasa ikizingatiwa chanjo imekuja mapema, hayo yote yakazingatiwa kabla ya kukubali chanjo
NB Maana yake maswali anayoyauliza leo Rafiki yangu baba askofu ni maswali ambayo serikali yetu iliyauliza kwenye jamii ya kisayansi duniani wiki ya pili tu baada ya hizi chanjo kutangazwa.
Aidha maswali haya anayouliza leo Ndugu yetu Mhe. Gwajima ametohoa kwenye majibu yetu kwanini tulikataa kupokea chanjo mapema. Mhe. Baba Askofu Gwajima yuko nyuma sana, anayoyasema leo yalikuwa kwenye mdahalo wetu zaidi ya mwaka mmoja uliopita wakati chanjo ikiwa na siku tatu tuu toka kutangazwa.
Post a Comment