MHE. KUNDO AKABIDHI VIFAA VYA TEHAMA SHULE 6 SHINYANGA
Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Mhandisi Kundo Mathew amekabidhi vifaa vya TEHAMA kwa ajili ya shule 6 za Sekondari zilizopo ndani ya Mkoa wa Shinyanga vyenye thamani ya shilingi Milioni 50 vilivyotolewa na Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF)
Makabidhiano hayo yamefanyika tarehe 14.08.2021 Mkoani Shinyanga kati ya Naibu Waziri huyo na Mbunge wa viti maalum wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Janista Mboneko, na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Shinyanga Nice Munisi ambapo jumla ya kompyuta 30 na printa 4 zilikabidhiwa rasmi
Akizungumza mara baada ya makabidhiano hayo Mhandisi Kundo amesema kuwa Serikali kupitia UCSAF imeendelea kutekeleza mradi wa kupeleka vifaa vya TEHAMA katika shule za umma ili kuchochea ukuaji wa matumizi ya TEHAMA na kuwaandaa vijana na mabadiliko ya teknolojia duniani
Sambamba na hilo amezungumzia mradi wa wasichana na TEHAMA unaotekelezwa na UCSAF ambao unalenga kuwawezesha na kuwajengea uwezo watoto wa kike katika TEHAMA ndio maana katika upelekaji wa vifaa vya TEHAMA katika shule za sekondari Mfuko huo unaangazia na Shule za Sekondari za wasichana
“Wizara kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote tuna kipengele kingine cha kuwawezesha watoto wa kike na TEHAMA ili kuwajengea uwezo na hatimaye kutengeneza wataalam wa TEHAMA wengi zaidi nchini kwa sababu mpaka sasa wataalam wa TEHAMA wanawake ni wachache kuliko wa kiume lengo letu ni kwamba tunapoongelea 50 kwa 50 ionekane kwa vitendo”, amesema Mhandisi Kundo
Katika hatua nyingine Mhandisi Kundo huyo ameushukuru uongozi mzima wa Mkoa wa Shinyanga kwa kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Wizara hiyo huku akimtaja Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Philemon Sengati na wasaidizi wake ambao wamekuwa ni chachu ya mtazamo chanya katika kukuza matumizi ya TEHAMA nchini

Post a Comment