Advertisement

Responsive Advertisement

ACT WAZALENDO WAMPONGEZA RAIS HAKAINDE HICHILEMA

Taarifa ya Idara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ya ACT Wazalendo imempongeza Ndg. Hakainde Hichilema kwa kuchaguliwa kuwa Rais mpya wa Jamhuri ya Zambia.

"Kwa kuzingatia matokeo rasmi yaliyokwishatangazwa na Tume ya Uchaguzi ya Zambia (ECZ) na baada ya Rais Edgar Lungu kukiri kushinwa ni dhahiri kuwa Ndg. Hakainde Hichilema ambaye ni mgombea wa chama cha UPND amevuka wigo wa zaidi ya asilimia 50 (50%+1) ya kura zote na hivyo kushinda uchaguzi mkuu na kumuacha mbali mgombea aliyekuwa akitetea nafasi hiyo ya Urais, Ndg. Edgar Chagwa Lungu"

"Sisi ACT Wazalendo tukiwa ni Chama kiongozi wa Upinzani nchini Tanzania na Chama rafiki wa Chama cha UPND, tunampongeza Ndg. Hakainde Hichilema kwa kuchaguliwa Rais wa 7 wa Jamhuri ya Zambia"

"Ni matumaini yetu kuwa, chini ya uongozi wa Hakainde Hichilema, nchi zetu mbili- Tanzania na Zambia, zitashamirisha na kuimarisha uhusiano wa kihistoria katika nyanja za kiuchumi, miundombinu, na kikanda kupitia Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).

"Tunakutakia mafanikio katika majukumu yako mapya ya kuitumikia Zambia na hivyo kutimiza matakwa ya wananchi wa Zambia."---- ACT-WAZALENDO

Post a Comment

0 Comments