Advertisement

Responsive Advertisement

AMKA NA BWANA LEO 16

*KESHA LA ASUBUHI.*

Jumatatu, 16/08/2021.

*JE! UNAWEZA KUDAI MUHURI WA MUNGU?*

*Enyi watu wangu, sikilizeni sheria yangu, Tegeni masikio kwa maneno ya kinywa changu. Zaburi 78:1.*

▶️Tunao ujumbe wa kupeleka kwa wale ambao hawajapata nuru ya ukweli wa leo, na katika kazi yetu hatupaswi kuikana imani yetu. Uchunguzi wa historia ya wana wa Israeli utatusaidia kujifunza masomo ambayo yatatuzuia kurudia  makosa yaliyoharibu rekodi yao. Bwana kwa namna ya ajabu aliwakomboa watu hawa kutoka katika utumwa wa mfalme mnyanyasaji, na Yeye mwenyewe akachukua madaraka juu ya jeshi lao kubwa. Aliwaongoza kwa nguzo ya wingu wakati wa mchana, na nguzo ya moto wakati wa usiku—wingu ambalo lilifunika uwapo Wake mwenyewe. Aliwapa chakula jangwani; na watu walikula chakula cha malaika....

▶️Mara tu baada ya Israeli kupiga kambi huko Sinai, Musa aliitwa kwenda mlimani kukutana na Mungu. Akiwa peke yake alipanda njia yenye mwinuko mkali na mawe yaliyochongoka, na kulisogelea na wingu lililoashiria mahali pa uwapo wa Yehova. Israeli  sasa ilikuwa ichukuliwe katika uhusiano wa karibu na wa kipekee na Mungu Aliye Juu. Kama taifa walipaswa kuwa chini ya serikali maalumu ya Mungu....

▶️Katikati ya ngurumo na radi Mungu alitamka sheria yake umati mkubwa huo ukisikia. Mungu alilipa tukio lile la kutolewa kwa sheria moja ya utukufu wa kutisha. Alitaka sana watu wapate kuelewa sifa bainishi ya juu ya sheria yake. Watu lazima wafundishwe kwamba kila kitu kilichohusiana na huduma Yake ni lazima kizingatiwe kwa heshima kubwa....

▶Muda uliobaki kwa ajili yetu ni mfupi sana. Hebu tuondoe kuendekeza nafsi kote; kwa kuwa huku kunadhoofisha nguvu ya kimwili, kiakili, na ya kimaadili, na kumfanya wakala wa kibinadamu kushindwa kuwa na maana ya kweli ya utakatifu anaotaka Mungu....

▶️Je mnaweza kustahili muhuri wa Mungu aliye hai? Je mnaweza kudai kwamba mmetakaswa kwa ukweli? Kama kanisa, hatujaipa sheria ya Mungu sifa yake kama tulivyopaswa kufanya. Tuko katika hatari ya kufanya starehe zetu wenyewe katika siku ya Sabato.

▶️ *Mafundisho ya thamani yametolewa kwa watu wetu katika vitabu ambavyo nimeamriwa kuandika. Ni wangapi wanasoma na kuvichunguza vitabu hivi? Nuru ambayo Mungu ameitoa inaweza kuangaliwa kwa kutojali na kutokuamini, lakini nuru hii itawahukumu wote ambao hawajachagua kuikubali na kuitii.*

*MUNGU ATUBARIKI SOTE.*
🙏🙏🙏🙏

Post a Comment

0 Comments