MADHARA YA KUINGIA KWENYE NGONO KABLA YA NDOA
*MADHARA YA KUINGIA KWENYE NGONO KABLA YA NDOA:*
*Na Mch.Mkama*
Ikumbukwe kuwa ‘familia moja iliyo na nidhamu na utaratibu mzuri, huwa na mvuto wa nguvu zaidi kwa niaba ya ukristo (kuuelezea ukristo) kuliko mahubiri yote yanayoweza kuhubiriwa’, (Adventist Home uk 32)
Vijana wengi leo wamejiingiza kwenye mambo ya ngono kabla ya kuunganishwa katika ndoa takatifu huu sio mpango wa Mungu na imechangia ndoa nyigi kutokua na uaminifu kwani mwovu anapoleta changamoto watu hukumbuka maisha ya zamani na kuingia katika dhambi.
Jambo hili limeleta madhara makubwa na vijana wengi ni wahanga wa jambo hili yapo madhara mengi yanayotokana na kujiingiza kwenye ngono kabla ya muda kama yafuatayo.
*Kuomkosea Mungu: (Kutoka 20:14) , (Mwanzo 39:6-12)*
Mungu ametoa agizo usizini hivyo unapozini unamkosea Mungu hivyo unaanza safari ya kutembea bila Mungu katika maisha yako na ni rahisi kuanzisha safari ya dhambi zingine. (Mwanzo 39:6-12)
*Kudharauliwa/Kujuta/kuchukiwa.(2 Samweli 13:6-15)*
Watu watakudharau na hivyo heshima yako inashuka katika jamii rejea kisa cha Amnoni na Tamari baada ya tendo hilo Amnoni alimchukia sana Tamari.
*Kuchelewa kuolewa au kutooa kabisa*.
Vijana wa kiume na wakike hawapendi mtu mhuni hivyo watakudanganya tu na mwisho kila mmoja atakukimbia unaweza usiolewe au usioe kabisa kila mmoja atajihami kutokana na tabia yako.
*Kupata magonjwa ya kuambukiza/Ukimwi*
Yapo magonjwa mengi ya ngono ya kuambukiza na mengine ni mabaya sana epuka magonjwa haya kwa kuwa muaminifu wengine wamepoteza maisha hata hawajaingia kwenye familia kutokana na kutokua waaminifu.
*Kubeba mimba na kuzaa watoto wasio na malezi ya baba na mama.*
Wapo watoto ambao wamejikuta wakilelewa na watu wasio wazazi wao kwa sababu mbalimbali, pengine tokea utotoni. Ni ajabu kuwa wengine hata wakipata uelewa mzuri wa wazazi wao, na akili zao zikipambanua vizuri yawapasayo kufanya, huamua kukataa kuwa sehemu ya familia ya wazazi wao. Utasikia lugha ikisema,’ Nimezoea ujombani, hata sidhani kama nitakubalika kwao baba.’ Haseni nitakubalika kwetu, bali kwao baba. Yawezekana sana kuwa sababu zilizompeleka ujombani zilikuwa nzito kabisa. Kwa sasa amekua mtu mzima inabidi afanye.
Familia nyingi hazina amani kutokana na watoto wasio na baba kwani inabidi uanze mipango ya kuiba fedha ukiolewa ili umhudumie mtoto ulie muacha kwa wazazi wako.Kwa wanaume wakati mwingine hawasemi ukweli na muda ukifika wanaumleta mtoto nyumbani pasipo makubaliano hili linafanya nyumba kukosa furaha na uaminifu.
*Kutoa mimba,Kufa na mimba,Kutozaa kabisa akiolewa kwa madhara ya mimba alizotoa.*
Vijana wengi wamepoteza maisha wakati wanatoa mimba na wengine hawana watoto kwa sababu ya kutoa mimba wakati wa usichana wao kwani utoaji wa mimba sio mpango wa Mungu na wengi wanajishughulisha na kutoa nmimba hawana utaalamu hivyo unaweza kupata madhara makumbwa sana.
*Kufarakana na wazazi na marafiki na kanisa.*
Vijana wengi wakiambiwa waache ngono hawakubali hivyo kujenga mazingira ya ugomvi kati yao na wale wanaowaambia waache ngono utasikia huyu nae si afate mambo yake huyu madha au dingi ni mnoko sana natamani uhuru maneno haya husikika katika midomo ya vijana wengi mwisho wake yana madhara makubwa.
Kushindwa kutulia na mme mmoja au mke mmoja.
Ukishazoea kuwa na wapenzi wengi huwezi kutulia hivyo hata ukiolewa au ukioa ndoa yako haitakua na furaha.
*Kubadilishana vinasaba na kuchukua vinasaba vya magonjwa ya kurithi.DNA.* Mwanamke anachangia 20% na Mwanaume 5% hizi hubadilika kutokana na mfumo wa uaminifu kama wewe sio muaminifu vinasaba vyako vinabadilika kutoka kwa mwanamke au mwanaume mmoja kwenda kwa mwingine.
*Ngono za mtandao/Master beshen/kujichua*.
Kupunguza nguvu zah mwili uwezo wa akili katika kufikiri kuzalisha magonjwa ya kisaikolojia.(K/Torati 22:23-30)
Post a Comment