BASHUNGWA; KWANDIKWA ALINIKUMBUSHA KUSALI BUNGENI

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa amepokea kwa mshtuko taarifa ya kifo cha kaka yake comrade Elias Kwandikwa. 

Pamoja na wema na mazuri yote aliyoyafanya hapa duniani, Mhe. Bashungwa amesema hakumsahau Mungu. 

"----->Alikuwa akinikumbusha kila mara Bungeni kuacha majukumu mengine na kutenga muda wa kusali mle Bungeni kuna kanisa"----BASHUNGWA

Ametoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki na wote walioguswa na msiba huu.

No comments