AMKA NA BWANA LEO 30
*KESHA LA ASUBUHI*
Jumatatu Agosti 30, 2021
*UTAKASO WA DHATI*
*Akawaambia wote, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku, anifuate.* Luka 9:23
▶️ Mkutano wa jumatatu asubuhi ulianza saa kumi na Moja na nusu chini ya hema. Nilizungumza kwa takribani dakika thelathini juu ya umuhimu wa uangalifu Katika matumizi juu ya mavazi na matumizi ya mali. Kuna hatari ya kuwa mzembe na kutumia ovyo ovyo pesa za Bwana. Wachungaji vijana wanaojishughulisha na Kazi ya hema wanapaswa kuwa waangalifu na wasiwe na matumizi makubwa. Mahitaji ya kazi ya Mungu ni mengi, kadri mahema yanavyoingia katika viwanja vipya na kadri kazi ya umishonari inavyokua. Uangalifu makini zaidi wa matumizi unapaswa kutumika Katika jambo hili bila ubahili ....
▶️ Mkutano wetu wa asubuhi ulifanyika Katika hema. Nilizungumza tena kwa takribani dakika thelathini kuhusiana na utakaso wa kweli ambao si kingine ila kufa Kila siku kwa nafsi kutenda kila siku yanayokubaliana na mapenzi ya Mungu. Utakaso wa Paulo ulikuwa ni mapambano ya kila siku na nafsi. Alisema, "ninakufa kila siku" (1 Wakorintho 16:31). Mapenzi yake na matamanio yake kila siku yalipingana na wajibu na mapenzi ya Mungu, bila kujali ni kiasi gani hayafurahishi na yenye kusulubisha asili yake. Sababu ambayo inafanya wengi katika zama hizi za ulimwengu kutopiga hatua yoyote kubwa katika maisha matakatifu ni kwa kuwa wanatafsiri mapenzi yao wenyewe kuwa ndiyo yale Mungu anataka. Wanafanya vile hasa watakavyo na kujifurahisha kuwa wanapatana na mapenzi ya Mungu. Wanaipendeza nafsi katika kila kitu na hawana mgogoro na nafsi.
▶️ Wengi hupambana vyema mwanzoni dhidi ya tamaa za ubinafsi za anasa na starehe. Wao ni wakweli na wenye bidii, Lakini wanazichoka juhudi zile zinazoendelea za kifo cha kila siku, machafuko yasiyokoma ya kupinga majaribu ya shetani, na uvivu unaonekana ukiwavuta, kifo pia huchukua nafsi, nao hufumba macho yanayosinzia na kuanguka chini ya majaribu badala ya kuyapinga. Dhambi za
Post a Comment