AMKA NA BWANA LEO 27
*KESHA LA ASUBUHI*
*Ijumaa 27/08/2021*
*ULIMWENGUNI, LAKINI SI WA ULIMWENGU*
" _Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa Mungu._ "
Yakobo 4:4.
▶️ Siku kuu ya Bwana imekaribia kabisa. Kristo atakapotokea katika mawingu ya mbinguni, wale ambao hawakumtafuta kwa moyo wote, wale ambao wameruhusu wadanganywe, wataangamia hakika. Usalama wetu pekee unapatikana kupitia toba na uongofu, na kufutwa kwa dhambi. Wale ambao sasa watamtafuta Bwana kwa bidii, wakinyenyekeza mioyo yao mbele Yake, na kuacha dhambi zao, kupitia katika utakaso wa Ile kweli, wataandaliwa kwa ajili ya kuungana na washiriki wa familia ya kifalme, nao watamwona mfalme katika uzuri Wake. ...
▶️ Vyovyote yalivyo mafanikio yake ya kielimu, ni yule tu anayetambua uwabijikaji wake kwa Mungu, na ambaye anaongozwa na Roho Mtakatifu, ndiye anaweza kuwa mwalimu mzuri-mwenye kuleta matokeo yanayotakiwa, au mwenye kufanikiwa kuwaleta kwa Mungu wale ambao wanaletwa chini ya mvuto wake. Je, wale ambao4 hawatii ushauri wa kiungu wakubaliwe kuwa viongozi katika taasisi za Bwana? -La hasha. Tunawezaje kuwachukulia kuwa kama viongozi salama wale wanaodhihirisha roho ya kutokuamini, na ambao, kwa maneno na tabia, wanashindwa kudhihirisha utauwa wa kweli?
📚 “Amin nawaambia, Msipoongoka na kuwa kama vitoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni” (Mathayo 18:3).
▶️ Inabidi nafsi isalimishwe chini ya nira ya Kristo. Mwalimu mkuu anawaalika wote wajifunze kwake .... "Mwana wa Adamu alikuja kukiokoa kilichopotea" (aya ya 11). Lakini wale wanaotaka kuokolewa ni lazima wawe tayari kuokolewa kwa njia iliyochaguliwa na Bwana, na sio kwa njia waliyoichagua wao wenyewe. Neema ya bure ya Mungu ndio tumaini pekee la mwanadamu. Mungu ana ari na kila mmoja wetu ....
▶️ *Tumeitwa kuwa watu maalumu wa Bwana katika maana ya juu zaidi kuliko vile ambavyo wengi wametambua. Ulimwengu umelala katika uovu, na watu wa Mungu wanapaswa kutoka ulimwenguni, na kujitenga. Wanapasa kuwa huru kutokana na desturi na mienendo ya dunia. Hawatakiwi kukubaliana na maoni ya kidunia, bali wanapaswa kujitokeza kuwa tofauti, kama watu wa pekee wa Bwana, wenye bidii katika utumishi wao wote. Hawapaswi kuwa na ushirika wowote na kazi za giza.*
Post a Comment