SIMBA SC WAPATA SHAVU, KUWEKA KAMBI NCHINI MAREKANI
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Klabu ya Simba SC Mohamed Dewji "Mo" amekutana na mmiliki wa klabu ya mpira wa miguu ya DC United ambayo ina thamani ya dola za kimarekani millioni 700.
Mo ametangaza ushirikiano mpya kati ya klabu za DC United na Simba.
Ifikapo mwaka 2022, Mo amesema klabu ya Simba itasafiri kwenda nchini Marekani kwaajili ya mazoezi na maandalizi ya msimu mpya, na pia itashiriki katika mashindano ya kimataifa yatakayoandaliwa na klabu ya DC United, ambayo yatahusisha ligi ya MLS na vilabu kutoka Amerika ya Kusini.
Post a Comment