AL-SHABAB WAPONGEZA JUHUDI ZA TALIBAN

Vyombo vya habari vinavyojihusisha na kundi la wanamgambo wa Kiislamu lenye makao yake nchini Somalia al-Shabab vimefurahia kuanguka kwa serikali inayotambuliwa kimataifa ya Afghanistan na kupongeza Taliban kwa kuuteka nchi hiyo.

"Mungu ni mkubwa: mji wa Kabul unaangukia kwa majeshi ya Imarati ya Kiislamu", tovuti zinazounga mkono kundi la al-Shabab Calamada na Somali Memo zimeandika katika vichwa vya habari vilivyofanana.

"Sherehe zilianza kote nchini, huku bendera inayoashiria kuabudu Mungu mmoja ikipandishwa katika viwanja vikuu vya Kabul na picha zilizotolewa na Imarati wa Kiislamu zikionyesha mujahideen wakishika doria katika vitongoji vilivyo karibu na Kabul wakati maisha yanarejea katika hali ya kawaida", Calamada.com imeripoti.

Ripoti hiyo imesema kuwa Taliban wameshinda viongozi vibaraka wa "Afghanistan" na "mamia ya maelfu ya wanajeshi wa kigeni" baada ya miaka 20 ya kupigania jihadi.

Al-Shabab ina uhusiano na al-Qaeda na imekuwa ikipiga vita vikosi vya Somali vyenye kuungwa mkono na Umoja wa Afrika tangu katikati ya miakaya 2000.

Wakati kutwaliwa kwa mji mkuu wa Afghanstan kumeikera Marekani na washirika wake, ambao wameitoroka nchi hiyo, Uchina na Urusi zimeonesha kuwa hazina mpango wa kufunga balozi zake nchini Afghanistan.

Uchina imewatahadharisha raia wake waliopo nchini Afghanstan kutoenda popote, bali waendelee kuwepo, lakini ikasema inafanya mazungumzo na maafisa mbali mbali wa Afghanstan kuhakikisha raia wake wanalindwa.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi aliviambia vyombo vya habari Jumapili kwamba serikali haina mpango wowote wa kuwaondoa raia wake Afghanstan.

Mwishoni mwa mwezi Julai, maafisa wa Taliban walifanya ziara nchini Uchina na kukutana na waziri wa mambo ya nje wa Uchina Wang Yi.

Wakati huo mkutano huo ulielezewa kama wa kuwatambua Taliban kama serikali.

Wizara ya mambo ya nje ya Uchina inasema ‘’hakutakuwa na tofauti" yoyote katika masuala ya ndani ya Afghanstan.

No comments