YOUTUBE YAFIKISHA WAPAKUAJI (DOWNLOADS) BILIONI 10

Application ya youtube imeingia kwenye orodha ya kuwa app ya kwanza iliyovunja rekodi nakuongoza kwa kuwa application pekee ilio pakuliwa  mara nyingi zaidi duniani kwenye vifaa vya android (yaani the most downloaded app) ambapo inaelezwa mtandao huo umepakuliwa zaidi ya mara bilioni 10 duniani kote kupitia google play store.

Idadi hii ya watu waliodownload mtandao wa youtube kiuhalisia imezidi kiwango cha makadirio ya idadi halisi ya watu wote dunia.

Na hapo ndipo unapozaliwa utata unaoibua maswali mengi kuwa inawezekanaje mtandao huo ukawa umepakuliwa mara bilioni 10 wakati makadirio ya idadi ya watu wote ulimwenguni ni bilioni 7.9?.

wataalamu wanaeleza kuwa idadi hii ya downloads bilioni 10, inakuja kufuatia namna ya matumizi ya diveces yanavyoongezeka na kiuhalisia inatokana na utaratibu uliopo kwa baadhi ya watu wengi kununua mobile devices mpya, yaani watu wengi huwa na vifaa kama simu au computer zaidi ya moja na kila kifaa kinakuwa na application hiyo ya youtube, na pia wapo maelfu ya watu ambao walifariki wakiwa ni watumiaji wa application hiyo, hivyo waliacha vifaa vyao vikiwa tayari vimepakua application hiyo pendwa na maarufu duniani, kitu kinachosababisha ongezeko la namba za downloads na kuifanya kuingia kwenye rekodi ya kuwa application kutoka playstore inayoongoza kwa downloads nyingi zaidi ulimwenguni kwa sasa .

YouTube ni mtandao wa kijamii  unaohusisha kushiriki/ku-share maudhui yaliyo katika mfumo wa video ulionzishwa rasmi february 2005 chini vijana watatu ambao ni Steve Chen, Chad Hurley, na Jawed Karim,  na mpaka sasa inaelezwa baada ya Google, YouTube ndio wavuti/website inayotembelewa zaidi ulimwenguni.

No comments