YANGA SC WAACHANA NA NAHODHA LAMINE MORO

Uongozi wa Klabu ya Yanga umetoa shukrani za dhati kwa Lamine Moro kwa utumishi wake ndani ya klabu ya Yanga katika kipindi cha miaka miwili.

Lamine Moro ambaye pia amekuwa nahodha kwa msimu huu, na kwa pamoja pande zote mbili wamekubaliana kusitisha Mkataba wake.

Hivyo basi Klabu ya Yanga inamtakia Lamine Moro kila la heri katika maisha mapya ya mchezo wa soka huko aendako.

No comments