AMKA NA BWANA LEO 29

*KESHA LA ASUBUHI.*

Alhamisi, 29/07/2021.

*AHADI YA MUNGU KWA WAZAZI.*

*Wana wetu na wawe kama miche Waliokua ujanani. Binti zetu kama nguzo za pembeni Zilizonakishwa kwa kupamba hekalu. Zaburi 144:12.*

▶️Tumechukuliwa kama mawe yanayoparuza kutoka katika machimbo ya ulimwengu kwa kisu cha ukweli na kuwekwa kwenye karakana ya Mungu. Yeye aliye na imani ya kweli katika Kristo kama Mwokozi wake binafsi, atagundua  kwamba ukweli unafanya kazi dhahiri kwa ajili yake. Imani yake ni imani itendayo kazi, na imani hutenda kazi kwa upendo, na kuisafisha roho. Bwana Yesu amelipa pesa ya fidia kwa ajili yetu; Ametoa maisha yake mwenyewe ili wale wanaomwamini wasipotee, bali wawe na uzima wa milele. Wale wanaopokea ukweli kwa imani watatoa ushuhuda wa ubora wa imani waliyo nayo. Daima wataendelea kufanya vizuri zaidi, huku wakimwangalia Yesu ambaye ndiye Mwanzilishi na Mkamilishaji wa imani yetu. Hatuwezi kuunda imani yetu; lakini tunaweza kuwa wafanya kazi pamoja na Kristo katika kukuza ukuaji na ushindi wa imani....

▶️Kazi ya Kristo moyoni haiharibu nguvu za mwanadamu. Kristo anaongoza, anaimarisha, anaadilisha, na kutakasa uwezo wa roho. Ni kupitia uzoefu binafsi naye ndipo tunapostahili kuwakilisha tabia yake kwa ulimwengu. Yohana anasema, "Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake" (Yohana 1:12). Na tena, "Kwa kuwa katika utimilifu wake sisi sote tulipokea, na neema juu ya neema" (aya ya 16).

▶️ *Kristo sharti awakilishwe katika familia nyumbani. Akina baba na akina mama hubeba jukumu zito; kwani watawajibishwa kwa ajili ya kutoa masomo sahihi kwa watoto wao. Wanapaswa kuzungumza nao kwa wema, kuwa wavumilivu kwao, kukesha na kuomba, kumwomba Bwana aunde mioyo ya watoto hao. Lakini wakati tunamwomba Mungu kuunda na kunyoosha na mioyo ya watoto hawa, hebu mama na baba watekeleze sehemu yao, wakiwasilisha kwa watoto wao uwakilishi hai wa Mfano wa mtakatifu. Mungu hatakubali kazi ya ovyo ovyo kutoka katika mikono yako. Watoto wako ni urithi wa Mungu, na malaika wa mbinguni wanaangalia kuona kuwa wazazi na watoto wote ni watenda kazi pamoja na Mungu katika kujenga tabia kulingana na mfano wa kiungu.*

*MUNGU ATUBARIKI SOTE.*

No comments