WANANCHI WAFANYA VURUGU, WATAKA JACOB ZUMA ATOKE
Serikali ya Afrika Kusini imepeleka wanajeshi kukabiliana na machafuko mabaya yaliyotokana na kufungwa kwa Rais wa zamani Jacob Zuma.
Maduka yameporwa na majengo yamechomwa moto leo Jumatatu na wananchi nchini humo baada ya Zuma kuhukumiwa na Mahakama kifungo cha miezi 15 Jela.
Watu wasiopungua sita wameuawa na 200 wamekamatwa tangu machafuko hayo yaanze wiki iliyopita, baada ya Zuma kujikabidhi na kuanza kifungo chake cha miezi 15.
Zuma alihukumiwa kwa kudharau Mahakama baada ya kukosa kuhudhuria uchunguzi wa ufisadi wakati wa Urais wake.
Mpaka sasa, wataalam wa sheria wanasema nafasi yake ya Kufaulu/Kushinda kesi yake ni ndogo.
Aidha, wataalam hao wamesema Kesi hiyo imesababisha mchezo wa kuigiza wa kisheria nchini Afrika Kusini, ambao haujawahi kuona Rais wa zamani akifungwa jela.
Post a Comment