MOTO ULIOZUKA KASULU-KIGOMA LILIKUWA NI JARIBIO TUU
NMB yakanusha taarifa zilizokuwa zikienea mitandaoni zikionyesha Jengo la NMB, lililoko Wilayani Kasulu mkoani Kigoma likiungua moto, wasema lilikuwa ni jaribio.
Wamefanya jaribio la kupima utayari wa kukabiliana na janga la moto (Fire Drill) katika tawi la Kasulu, Kigoma.
Wamethibitisha kuwa, zoezi hili limefanyika ili kupima utayari wa wafanyakazi, wateja na wadau muhimu katika kukabiliana na majanga ya moto.
Aidha, NMB imesema zoezi limeenda vizuri na hakuna madhara yoyote yaliyojitokeza katika tawi hilo; huduma zimerejea kama kawaida.
Post a Comment