NENO KUU LEO MAKAMBINI 12

MAKAMBI MWENGE 2021. POPOTE NA YESU NITAKWENDA.

*JULAI 11, 2021
*MNENAJI: 
*Mch. Godwin Lekundayo NTUC

Yoshua 4:1-11

Ikiwa hapo hilo taifa zima lilipokuwa limekwisha vuka Yordani, ndipo Bwana akanena na Yoshua, akamwambia, 

2 Haya, twaeni watu waume kumi na wawili katika hao watu, kila kabila mtu mmoja, 

3 kisha uwaamrishe, kusema, Twaeni mawe kumi na mawili, hapo katikati ya Yordani, mahali hapo miguu ya hao makuhani iliposimama imara, mwende nayo mawe hayo, mkayaweke nchi kambini, hapo mtakapolala usiku huu. 

4 Basi Yoshua akawaita hao watu kumi na wawili, aliokuwa amewaweka tayari tangu hapo, katika wana wa Israeli, kila kabila mtu mmoja; 

5 naye Yoshua akawaambia, Haya, piteni ninyi mtangulie mbele ya sanduku la Bwana, Mungu wenu, mwende pale katikati ya Yordani, mkatwae kila mtu wenu jiwe moja begani mwake, kwa kadiri ya hesabu ya kabila za wana wa Israeli; 

6 ili kwamba jambo hili liwe ishara kati yenu, hapo watoto wenu watakapowauliza ninyi katika siku zijazo, wakisema, Ni nini maana yake mawe haya? 

7 Ndipo mtakapowaambia, Ni kwa sababu maji ya Yordani yalitindika mbele ya sanduku la agano la Bwana; hapo lilipovuka Yordani, hayo maji ya Yordani yalitindika; na mawe haya yatakuwa ni ukumbusho kwa wana wa Israeli milele. 

8 Basi wana wa Israeli walifanya vile vile kama Yoshua alivyowaamuru, nao wakatwaa mawe kumi na mawili pale katikati ya Yordani, kama Bwana alivyomwambia Yoshua, sawasawa na hesabu ya kabila za wana wa Israeli; wakayachukua wakavuka nayo hata mahali pale walipolala, nao wakayaweka nchi kuko huko. 

9 Kisha Yoshua akapanga mawe kumi na mawili katikati ya Yordani, mahali pale miguu ya hao makuhani waliolichukua hilo sanduku la agano iliposimama; nayo yapo pale pale hata hivi leo. 

10 Kwa kuwa makuhani waliolichukua hilo sanduku walisimama katikati ya Yordani, hata mambo yote Bwana aliyomwamuru Yoshua awambie hao watu yakaisha, sawasawa na hayo yote Musa aliyokuwa amemwamuru Yoshua; kisha hao watu wakafanya haraka wakavuka. 

11 Ikawa watu wote walipokuwa wamekwisha vuka kabisa, hilo sanduku la Bwana likavuka, na hao makuhani, mbele ya macho ya hao watu.

19  Na watu hao wakapanda kutoka katika Yordani siku ya kumi ya mwezi wa kwanza, wakapiga kambi kule Gilgali+ kwenye mpaka wa mashariki wa Yeriko.

20  Kisha Yoshua akapanga katika Gilgali yale mawe kumi na mawili, ambayo walikuwa wamechukua kutoka katika Yordani.

21  Naye akawaambia wana wa Israeli: “Wana wenu watakapowauliza baba zao wakati ujao, wakisema, ‘Mawe haya yanamaanisha nini?’

22  Ndipo mtakapowajulisha wana wenu, mkisema, ‘Israeli walivuka huu mto Yordani ukiwa nchi kavu,

23  Yehova Mungu wenu alipoyakausha maji ya Yordani mbele yao mpaka walipokwisha kuvuka, kama vile Yehova Mungu wenu alivyokuwa ameifanya Bahari Nyekundu alipoikausha mbele yetu mpaka tulipokwisha kuvuka;

24  ili watu wote wa dunia wapate kuujua mkono wa Yehova, kwamba ni wenye nguvu; ili mpate kumwogopa Yehova Mungu wenu sikuzote.’”

👂kwa kawaida mwanadamu anakawaida ya kusahau ndiyo maana Mungu anamtaka mwanadamu mwanadamu aweke kumbukumbu

👀"kisha Yoshua akawaambia: “Piteni mbele ya sanduku la Yehova Mungu wenu mpaka katikati ya Yordani, na mjichukulie kila mmoja wenu jiwe moja begani mwake, kulingana na hesabu ya makabila ya wana wa Israeli, 6  ili kwamba jambo hili liwe ishara katikati yenu"

Sababu kuu ya hawa watu kuagizwa kila mtu kutwaa jiwe ilikuwa ni

1.kuwaelewesha watoto wao
2.watu wote wa dunia hii wapate kujua uweza wa Mungu (liwe hubiri)

Weka kumbukumbu

No comments