WALIOMUUA RAIS WA HAITI BAADHI WALIKUWA WAPELELEZI
Watu Kadhaa waliofungwa kwenye mauaji ya Rais wa Haiti Jovenel Moise inasemekana walikuwa wapelelezi wa zamani wa sheria za Marekani, mamlaka ya Marekani imethibitisha.
Takribani mtuhumiwa mmoja alifanya kazi na Wakala wa Utekelezaji wa Dawa za Marekani (DEA) kama mtoa habari anayelipwa. Wengine wanasemekana wanaweza kuwa na uhusiano na FBI.
Aidha, mamlaka ya Haiti imesema watu wasiopungua 28 walioajiriwa kupitia kampuni ya usalama yenye makao yake Florida walikuwa sehemu ya mapigano ambayo yalimuua Rais wa Haiti Jovenel Moise ambae aliuawa Jumatano iliyopita.
Post a Comment