UMMY MWALIMU AZIPONGEZA SHULE ZA SERIKALI FORM 6

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Charles Msonde ametangaza matokeo ya kidato cha sita mwaka 2021 na kutaja Shule kumi bora zilizofanya vizuri katika mtihani huo ambapo Shule iliyoshika nafasi ya kwanza kitaifa ni Kisimiri ya Arusha yenye Watahiniwa 72.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Ummy Mwalimu amezipongeza Shule za Serikali kwa kuchukua nafasi nyingi zaidi katika Kumi bora ya kwanza ikiwa ni;- Kisimiri (Serikali), Kemebos (Binafsi), Dareda (Serikali), Tabora Girls (Serikali), Tabora  Boys (Serikali), Feza Boys (Binafsi), Mwandet (Serikali), Zakia Meghji (Serikali), Kilosa (Serikali), Mzumbe (Serikali).

"Hakika uwekezaji uliofanywa na Serikali katika Sekta ya Elimu umeanza kuzaa Matunda"

"Shule zilizoitwa za Kata zimeonyesha matokeo makubwa kama vile Kisimiri, Dareda, Mwandet na Zakia Meghji! Hongereni sana Walimu na wanafunzi."--- UMMY MWALIMU

No comments