UKRAINE WARUHUSU JESHI LA KIKE KUVAA VIATU VIREFU

Wizara ya Ulinzi ya Ukraine imetetea uamuzi wake wa kufundisha wanajeshi wa kike kuandamana kwa kuvaa viatu vyenye visigino virefu kufuatia kilio kutoka kwa wabunge wa eneo hilo. 

Wanawake kutoka vikosi vya jeshi la Ukraine wataandamana katika gwaride kuadhimisha miaka 30 ya uhuru kutoka kwa Umoja wa Kisovyeti mnamo Agosti 24, kulingana na Jeshi Inform, wakala rasmi wa habari wa wizara ya ulinzi.

No comments