SERIKALI YAZITAKA SALUNI KUWAPIMA WATEJA JOTO

Wamiliki wa Saluni na Vinyozi wanatakiwa kuwa na vifaa vya unawaji mikono nje ya saluni ambapo kila atakayeingia katika eneo hilo atahitajika kunawa mikono au kutumia vitakasa mikono

Hakikisha uwepo wa taulo za kutosha zilizofuliwa, kukauka na kupasiwa kulingana na wingi wa Wateja. Kila Mteja atumie taulo lake lililo safi na pale ambapo Wateja huvishwa joho la kufunika mwili, Mhudumu ahakikishe mteja amezungushiwa tissue shingoni kabla ya kumvika joho hilo

Hakikisha hakuna msongamano wa Watu na kwamba kila kiti kiwe katika umbali wa mita moja na kuendelea na pale inaposhindikana wateja wasubiri nje. Hakikisha uvaaji wa barakoa muda wote kwa Watoa Huduma na Wateja

No comments