RAIS SAMIA AWATOA HOFU WATANZANIA, TOZO ZA MIAMALA

Rais Samia Suluhu Hassan amesema makato ya tozo za miamala iliwekwa kwa nia njema lakini kutokana na Serikali yake kuwa sikivu na kuwepo kwa vilio vingi, wameendelea kupokea maoni na wanatarajia kupokea taarifa ya kamati iliyoundwa ili kuweza kufikia njia nzuri na muafaka wa kuweza kulitatua kwa manufaa ya nchi.

"----->Lengo la makato hayo lililenga kuwanusuru wakulima wengi walioko vijijini wanaoteseka na ubovu wa miundombinu na hivyo kushindwa kunufaika na mazao yao hivyo fedha itakayopatikana kutokana na makato ya tozo hizo zitasaidia ujenzi barabara vijijini."---- RAIS SAMIA

No comments