PROF. MKUMBO AZINDUA BODI YA WAKURUGENZI TBS

Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo ameitaka Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kutengeneza mikakati ili kufikia malengo ya Shirika kwa kusimamia viwango na vigezo vya kupima utendaji wa Menejimenti, kutoa au kushiriki kutoa maamuzi wakati Shirika linakabiliwa na changamoto za kimenejimenti na mawazo mapya ya kuboresha uendeshaji wa shirika na kuhakikisha inaendelea kuwa kwenye ubora wake.

Ameyasema hayo Julai 8,2021 wakati wa akizinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Viwango Tanzania walioteuliwa 29 Juni 2021, ambapo amewasisitizia kujikita kwenye majukumu yao ili wasiingiliane na Menejimenti kwenye utendaji kazi.

Aidha, Waziri Prof. Mkumbo ameihasa Bodi hiyo kuwa na mahusiano chanya na yenye tija kati ya Bodi, Menejimenti na Serikali, huku akimtaka kila mmoja kuelewa majukumu yake sawa sawa na wajumbe kujiepusha na kufanya kazi za Menejimenti, Ushirikiano, kuthaminiani, kusikilizana, upendo na kuelewa vizuri maana, malengo, na majukumu ya Shirika, pamoja na sheria na kanuni zinazoendesha Shirika.

Waziri Prof. Mkumbo ameiomba Bodi hiyo kuanza na viporo vilivyopo katika kutatua changamoto kwenye Taasisi ikiwemo pamoja na suala la TBS kufanya kazi ya kuweka vinasaba, uamuzi wa kuanza kufanya ukaguzi wa magari yanayoagizwa kutoka nje hapa hapa nchini, lakini pia suala la wafanyabiashara wadogo kuona ni jinsi gani watatoa kwa urahisi alama za ubora kwa wafanyabiashara kwa kushirikiana na SIDO.

Naye, Mwenyekiti wa Bodi Wakurugenzi ya Shirika la Viwango Tanzania, Dkt Fenella Mukangara amehaidi kufanya kazi kwa bidii kwa kutatua changamoto zote na kuahidi kuwa msikivivu na kuishauri manenjimenti na kuhakikisha taasisi hiyo inatekeleza majukumu yake kikamilifu.

No comments