PONGEZI ZATOLEWA KWA WADAU WA MAENDELEO

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Ng’wilabazu Ndatwa Ludigija, amewapongeza wadau wa maendeleo kupitia mashirika ya USAID na PACT kwa kuunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuboresha ustawi wa jamii kwa kuwawezesha watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
 
Mhe. Ludigija alitoa pongezi hizo katika viwanja vya vya Karemjee jijini Dar es Salaam, wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa kwa ajili ya kuwawezesha watoto wanaoshi katika mazingira magumu pamoja na kugawa vifaa vya kuanzia biashara kwa vijana wajasiliamali 605 wanaotoka katika mazingira magumu, baada ya kuhitimu mafunzo katika fani mbalimbali kupitia VETA.
 
“Niwapongeze sana USAID kupitia shirika la PACT kwa miradi ya kizazi kipya na ACHIEVE kwa kufadhili vijana hawa kwa kuwapa nyenzo muhimu zitakazoenda kubadilisha maisha yao na kuboresha ustawi wa jamii, alisema Ludigija.
 
Aidha Ludigija alieleza kuwa Rais ameonesha muelekeo mzuri katika kuboresha maisha ya watanzania ikiwa ni pamoja na watoto wanaoishi katika mazingira magumu, hivyo aliwapongeza wadau hao kwa kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo.
 
Ludigija alisema kuwa Serikali kwa upande wake imeendelea kuorodhesha vijana na kuhakikisha kuwa wanapelekwa kwenye vyuo vya mafunzo ili wapate stadi za kazi ambazo zitawawezesha kujiajili na kujitegemea. “Serikali peke yake haiwezi kufanya yote, hivyo nitoe pongezi kubwa sana kwenu kwa hiki mnachokifanya,” alisema.
 
Vifaa vilivyokadidhiwa vinavyolenga kuisaidia Ofisi ya Rais Twala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) katika kutoa huduma kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu zaidi ni pamoja na; Viti 156, meza 57, makabati ya chuma 1033 na vifaa vingine vya utoaji taarifa ili kusaidia OR-TAMISEMI kazi za utoaji huduma kwa watoto wanaoshi katika mazingira hatarishi kupitia idara ya afya na ustawi wajamii.

Pia kupitia mradi wa ACHIEVE, ilielezwa kuwa zana zingine zipo katika hatua ya mwisho ya manunuzi ikiwemo gari 1, pikipiki 65, kompyuta mpakato 10, kompyuta za mezani 57,

No comments