• HOME
  • BREAKING NEWS
  • TAMTHILIA
  • MICHEZO
  • MATANGAZO
  • CONTACT US

BINAGO BLOG

  • Home
  • Home / MICHEZO / NA GEORGE AMBANGILE BELGIUM vs ITALY

    NA GEORGE AMBANGILE BELGIUM vs ITALY

    Bisaya Raphael July 03, 2021 MICHEZO
    Hii mechi hata ingekuwa fainali ni sawa tu . Watu wanapishana tu , njoo na mimi nije , ufundi, mbinu, kasi,nguvu , matumizi ya akili sana, kujituma na ufanisi wa daraja la juu

    ✍Roberto Mancini kafanya kazi kubwa sana uwanja wa mazoezi , na moja ya kazi yake ni upatikanaji wa goli la kwanza ( Counter Pressing ) mara tu baada ya Immobile kupoteza mpira ndani ya penalty box la Ubeligiji, Italy hawakurudi nyuma walianzia kukabia pale pale juu kwa presha kubwa na kupora mpira na goli likapatikana hapo. Well done !

    ✍Muundo wa Italia : kwenye football shape yao Italia tunaita " asymmetrical shape " kwamba haipo katika muundo uliosawa ( mfano mabeki wanne nyuma wapo katika muundo sawa ) lakini Italia Bonnucci na Chiellini wapo katikati halafu Di Lorenzo ambaye ndio beki wa kulia anabaki nyuma lakini mwenzake Spinazzola ndio anapewa uhuru wa kwenda mbele , akifanya hivyo winga wake Insigne anaingia ndani nyuma ya Immobile , halafu upande wa kulia Chiesa anabaki pembeni kule kule ( ndio shape ya asymmetrical ilivyo ) . Inasaidia nini ???

    ✍Insigne kuwa karibu na goli na pia nyuma ya Witsel na Tielemanns , mbili : inafungua njia kwa Spinazzola pembeni kushoto kukabiliana 1v1 na wingback wa Belgium , Tatu : inaongeza option nyingi za kupiga pasi kwenda mbele kutoka kwa Verratti na Jorginho lakini Nne : muhimu sana hii ...wakipoteza mpira wanakuwa takribani watano wa kuanza kufanya counter pressing .

    ✍Ubeligiji walim miss sana Eden Hazard leo , Jérémy Doku amecheza vizuri sana lakini bado hana ufundi wa Hazard hasa karibu na goli la timu pinzani, Hazars uwezo wake wa kucheza One-Two na wenzake na kuficha mpira unaleta shida sana kwa wapinzani , kwa kufanya hivyo huwa anakaribisha wachezaji wengi wamfuate na kufungua space kwa KDB na Lukaku .

    NOTE

    1: Bonucci + Chiellini maana halisi ya mabeki

    2: Jérémy Doku ana miaka 19 ana chumba kikubwa cha kuboresha zaidi kipaji chake. Kasi ya hatari

    3: JORGINHO ndio maana nimeandika herufi kubwa . Kiungo anayetumia akili nyingi sana aisee . What a player

    4: Gigi Donnarumma eti PSG wamempata bure daah


    Related Posts

    MICHEZO

    Post a Comment

    No comments

    Subscribe to: Post Comments ( Atom )

    KWA SHEREHE NA SEMINA KARIBU UKUMBI WA LAKE TANGANYIKA, NZEGA-TABORA

    FOOTBALL STORIES

    Follow us

    • Like on Facebook
    • Follow on Twitter
    • Follow on Instagram
    • Subscribe on Youtube

    Popular Posts

    • kusuka na unyoaji katika Biblia
      kusuka na unyoaji katika Biblia
       KAMA MUNGU ALIVYOKWISHA KUWAONYA WANAWAKE ! NDIVYO ALIVYOKWISHA KUWAONYA WANAUME PIA. BWANA YESU asifiwe!😅 Maranatha!😅🙏🏻 N...
    • Je kutoa Mahari ni sawa ktk biblia?
      Je kutoa Mahari ni sawa ktk biblia?
      *https://youtu.be/-P4s8sVq31o* 🤔🤔🤔🤔🤔 *JE NI HALALI KWA MKRISTO KULIPA MAHARI ILI AOE?????* 🤔🤔🤔🤔🤔 . . . Hebu tutazame k...
    • HII NDIO MISINGI YA KANISA LA WASABATO DUNIANI
      HII NDIO MISINGI YA KANISA LA WASABATO DUNIANI
      KANISA LA #SDA LINA MISINGI 28 AMBAYO NI 1.Neno la Mungu 2.Utatu mtakatifu 3.Mungu baba 4.Mungu mwana 5.Roho mtakatifu 6.Uumbaji...

    Labels

    Habari MICHEZO Live injili Tamthilia Kesha la Asubuhi BREAKING NEWS magazeti Matangazo Covid19 Mastaa Viongozi today's quote Lesoni leo Wimbo wa Leo barikiwa Je Wajua? KULFI Bongo Movies Stories TETESI ZA USAJILI

    Facebook

    Created By SoraTemplates | Distributed By Gooyaabi Templates