MAREKANI YASEMA NDEGE YA C-17 IMELETA MAHITAJI MUHIMU

Ndege iliyoonekana nchini na kuzua taharuki kwa Wananchi wengi, Marekani imesema ndege ya jeshi la nchi hiyo aina ya C-17 Globemaster iliyoegeshwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) imeleta mahitaji muhimu ya ubalozi wa nchi hiyo nchini Tanzania.

Ndege hiyo ambayo kwenye bawa lake la nyuma ina bendera ya Marekani chini yake ikiandikwa herufi AMC, picha zake zilianza kusambaa mitandaoni kuanzia juzi Alhamisi Julai Mosi, 2021 ikiwa katika uwanja huo uliopo jijini Dar es Salaam.

No comments