MWINYI AAHIDI KUTOA MILIONI 50 MSIKITI WA FISSABILILAH

Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameahidi kuchangia shilingi Milioni hamsini (50,000,000), kusaidia ujenzi wa Msikiti wa Jumuiya ya Fissabilillah Tabligh Markaz unaotumika kwa shughuli za Ijitmai.

Rais Mwinyi ameukagua Msikiti huo ambao bado unajengwa kwa nguvu za wananchi na baaadae akaweka jiwe la msingi.

Aidha, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amezindua mradi wa madarasa manane na chumba cha waalimu katika shule ya Msingi Chaani, amesema Serikali itahakikisha kunakuwepo madarasa ya kutosha pamoja na walimu wenye sifa ili kufanikisha dhamira ya kutoa elimu bora.

"----->Serikali itajipanga kuhakikisha inakuwa na walimu wa kutosha katika masomo ya Sayansi (Hesabu, Chemistry na Physics) ili kuinua kwango cha ufaulu."---> MWINYI

Ameyasema hayo akiwa katika Ziara yake jimbo la Chaani, Mkoa wa Kaskazini kisiwani Zanzibar, leo 06/07/2021.

No comments