MUONGOZO WA KUJIFUNZA BIBLIA KWA WATU WAZIMA LEO 30

*LESONI LEO.*

Ijumaa, 30/07/2021.

Usomaji wa Biblia: Matendo ya Mitume 4.

 *JIFUNZE ZAIDI.*

“Kazi yako inapokuwia ngumu, unapolalamikia magumu na majaribu, unaposema kwamba huna nguvu ya kustahimili majaribu, kwamba huwezi kushinda kukosa subira, na kwamba maisha ya Kikristo ni kazi ngumu sana, tambua kwamba haujajitia nira ya Kristo; umejitia nira ya bwana mwingine.” —Ellen G. White, Child Guidance, uk. 267.

“Kuna hitaji la kuwa na uangalifu wa kudumu na wa dhati, kupenda ibada, bali haya yatakuja kwa asili wakati nafsi inahifadhiwa kwa nguvu ya Mungu kupitia imani. Hakuna tunaloweza kufanya, hakuna kabisa, kustahili majaliwa ya Kiungu. Hatupaswi kabisa kujitumainia wenyewe au matendo yetu mema; bali tunapopotoka, viumbe wenye dhambi tunakuja kwa Kristo, tunaweza kupata pumziko katika pendo lake. Mungu atampokea kila mmoja ajaye kwake kwa kutegemea kabisa kustahili kwa Mwokozi aliyesulubiwa. Upendo huchipua katika moyo.

…. Yawezekana kusiwepo na furaha za hisia, bali kuna tumaini tulivu la kudumu. Kila mzigo ni mwepesi; kwa kuwa nira ambayo Kristo anaiamuru ni laini. Jukumu linakuwa jambo la kupendeza na kafara inakuwa furaha. Njia ambayo kabla ilionekana kughubikwa katika giza inakuwa angavu kwa miali itokayo katika jua la haki. Huku ni kutembea nuruni kama vile Kristo alivyo nuruni.” —Ellen G. White, Faith and Works, uk. 38, 39.

Masawali ya Kujadili

1. Je, unakumbuka wakati fulani katika kutembea kwako na Yesu ambapo mwisho kabisa ulijisalimisha? Shiriki wakati huu katika darasa lako na kujikita hasa katika sababu iliyofanya ujisalimishe.

2. Soma ombi la Yesu katika Mathayo 11:25—27 na kujadili katika darasa lako namna tunavyopata maarifa ya neema... Kwa nini Mungu huficha mpango wa wokovu (“mambo haya”) kwa wenye hekima na akili na kuwafunulia watoto wachanga?

3. Kwa njia ya kivitendo, tunawezaje, kuwasaidia wale wanaotuzunguka wakisumbuka na mizigo yao kuja kwa Yesu na kupata pumziko? Tafakari zaidi juu ya wazo hili la kuwa “mpole na mnyenyekevu wa moyo.” Je, hiyo si vibaya kwa kujithamini kwa mtu? Je, hatupaswi kuhisi vizuri kuhusu sisi wenyewe, hasa mtu anayepambana na kutokujiamini binafsi vyovyote vile? Ni kwa vipi msalaba na kile msalaba unachowakilisha, hutusaidia kuelewa kile Yesu anachomaanisha kuhusu kuwa “mpole na mnyenyekevu?” Maana yake ni kwamba, katika uwepo wa msalaba, kwa nini upole na unyenyekevu ndio mitazamo pekee halisi inayofaa kuwa nayo?
🙏🙏🙏🙏

No comments