AMKA NA BWANA LEO 30

*KESHA LA ASUBUHI.*

Ijumaa, 30/07/2021.

*AHADI: NGUVU KWA AJILI YA SIKU.*

*Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa tabia ya Uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa. 2 Petro 1:4.*

▶️Ninatamani sana kuwa na nguvu za kimwili na afya, kuwa na usafi wa akili, ili niweze kutoa kwa Mungu huduma inayokubalika. "Si ninyi mlionichagua mimi," Kristo alisema,  "bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni" (Yohana 15:16).

▶️Neno limejaa ahadi za thamani sana. Nitakuwa na nguvu ya kuona, nitakuwa na nguvu ya ubongo, nitakuwa na usafi wa mawazo na mvuto wa Roho Mtakatifu, kwa sababu ninaomba kwa jina la Yesu. Mwokozi wa Thamani! Alitoa maisha yake kwa ajili yangu. "Jinsi zilivyo kuu utajiri na hekima na maarifa ya Mungu! Hukumu zake hazichunguziki, wala njia zake hazitafutikani! Maana ni nani aliyeijua nia ya Bwana? Au ni nani aliyekuwa mshauri wake? Au ni nani aliyempa yeye kitu kwanza, naye atalipwa tena? Kwa kuwa vitu vyote vyatoka kwake, viko kwa uweza wake, tena vinarejea kwake. Utukufu una yeye milele. Amina." (Warumi 11:33-36).

▶️Nina shauku sana na manufaa ambayo sisi sote tunaweza kuyapata kwa imani. Sasa ni fursa yetu ya kuficha maisha yetu pamoja na Kristo katika Mungu. Kila kitambo kidogo cha muda wetu ni cha thamani. Vipaji vya thamani tulivyokopeshwa na Mungu vinapaswa kutumika katika kazi Yake. "Wala ninyi si mali yenu wenyewe; maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu. (1 Wakorintho 6:19-20).

▶️ *Ndio, sisi ni urithi wa Bwana ulionunuliwa kwa damu. "Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lo lote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu" (1 Wakorintho 10:31). Hili Mungu analitaka kutoka kwa kila mtu ambaye atakuwa sehemu ya familia Yake katika ufalme wa mbinguni. Ubinafsi wote lazima ushindwe. Lazima tuwe wakweli kwa Mungu, wenye utiifu usioyumba kwa amri zake zote. Binadamu hutunga sheria, nao wana ari sana kwa ajili ya utekelezaji wake. Wakati uo huo wanakiuka sheria ya juu kabisa kutoka kwa Mtawala mwenye nguvu kuliko wote. Hii wanajaribu kuifanya kuwa tupu na batili. Wanampandisha hadhi mwanadamu juu ya Mungu. "Je! Nisiwapatilize kwa sababu ya mambo hayo? Asema Bwana" (Yeremia 5:9). Ndio, Mungu atamlipa kila mtu kulingana na matendo yake.*

*MUNGU ATUBARIKI SOTE.*
🙏🙏🙏🙏

No comments