MSAMAHA KATIKA MAHUSIANO

*MSAMAHA*
Hebu fikiria! Kuna umuhimu gani wa msamaha kama hakuna kosa?
 *Kama hatujawahi kukwazana , basi hatufahamiani.*[Mithali ya Kichina]. Kwa nini kufahamiana kunaongeza uwezekano wa kukwazana? Unapokuwa karibu na mtu aidha kimahusiano au kirafiki/ kuishi nyuma moja- *unagundua* vitu kumhusu ambavyo usingeweza kuvijua ukiwa mbali... *baadhi* ya vitu hivi vitakukera& Kwa kadri mnavyohusiana kwa ukaribu ndivyo mnavyoongeza uwezekano wa kukwazana. Kwa sababu mahusiano (kabla&baada ya ndoa) yanahusisha kufahamiana kwa ukaribu, ni busara kujifunza MSAMAHA.

*Kuomba:Samahani Vs Msamaha*: Nafikiri kusema samahani tu sio fundisho la biblia kwa sababu haishughuliki hasa na kosa. mf. Adamak anasema " Honey! samahani kwa kutokusikiliza wakati ukiongea na mimi."  Evak anajibu , " Unauhakika kuwa unaumizwa na ulinichofanyia! Wewe ni miongoni mwa wanaume wanaojua kuomba samahani kuliko wote niliowahi kukutana nao.!"  Adamak ameomba samahani lakini bado mgogoro umekolea. Unaposema *samahani tu* haitoshi kumuonesha mwenzio jinsi unavyochukulia uzito wa kosa. Unapomuomba mwenzio/rafiki *Msamaha*, unadhihirisha kuwa umejidhatiti kujirekebisha na matokeo yake unamfanya ajisikie salama kukuamini.[Lou Priolo(1999), The Complete Husband, p.72-73.Emphasis mine]--Kwa sasa tujifunze jinsi ya kusamehe, *wakati mwingine tutajifunza jinsi ya kuomba msamaha katika muktadha wa mahusiano.*

*Msamaha Kimaandiko:* Nini maana ya msamaha? kwa kigiriki cha Agano jipya msahama humaanisha kuachilia *{letting Go}* Tumeamriwa kusamehe , " ..kama na Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi." [Efe 4:32]. Kwani , Mungu anasameheje ili tufuate mfano wake? Mungu anasema , "Mimi , naam, mimii , ndimi niyafutaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe , *wala sitazikumbuka dhambi zako*.& na nitausamehe uovu wao , *wala dhambi yao sitaikumbuka tena*[Isa 43:25&Jer31:34]

*Subiri kidogo!* Mungu si anajua kitu? tena si anajua dhambi zetu ,hata zile ambazo bado hatujazitenda[Heb4:13]? Ndio , uko sawa! Sasa kama ndivyo , Biblia inamaanisha nini inaposema Mungu anatusamehe wala hakumbuki tena? Yaani , anasahauje kitu anachokijua?🧐 Biblia inaposema Mungu "anasahau" dhambi zetu , inamaanisha ukweli kwamba  *Mdhambi aliyetubu anaposamehewa hasa na Mungu, Mungu hazishikilii tena dhambi zilizotubiwa dhidi yake*. Badala yake zinahesabiwa juu ya Kristo ambaye *tayari* ameshalipa adhabu na kubeba hatia ya wadhambi kama mimi na wewe kupitia kafara yake ya upatanisho pale msalabani. *Dhambi iliyotubiwa haiumizi tena moyo wake na wala hamtendei aliyemsamehe kulingana na makosa ya kale yaliyotubiwa*. Kwa haki ya Kristo anakuwa kama hajawahi kutenda dhambi kamwe.

*Kwa hiyo*:  Kwanza kabisa msamaha ni ahadi. Kama Mung u anavyoahidi kutozishikilia dhambi za zilizotubiwa dhidi ya mdhambi aliyetubu na kuamini , ndivyo nasi imetupasa kuahidi *kutoshikilia makwazo dhidi ya wale tuliyowasamehe.* Unaweza kudhihirisha ahadi hii kwa kufanya mambo haya : - *1.Hautatumia kwazo ulilolisamehe dhidi ya uliyemsamehe au kumtendea kulingana na kwazo ulilolisamehe tayari. 2. Hautajadili kwazo ulilolisamehe na wengine. 3. Hautadumu katika kwazo ulilolisamehe badala yake utajikumbusha kuwa umemsamehe kama Mungu alivyokusmehe wewe.*[Lou Priolo , The Heart of Anger , p.179,180].....itaendelea.

*BWANA!Tunakuomba utukirimie nia& uwezo wa kusameheana katika jina la Yesu Kristo...AMEN*



                                                                                                                                            *PMC360:2021*

No comments