PHILIP MPANGO AKUTANA NA BI. MERIE-HELLEN LOISON

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Isdor Mpango amefanya mazungumzo na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Maendeleo ya Ufaransa (AFD) Bi. Marie-Hellen Loison Mazungumzo hayo yamefanyika Paris Nchini Ufaransa.

Mazungumzo baina ya pande mbili yalijikita kujadili masuala mbalimbali ya kukuza na kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Shirika hilo.

Katika mazungumzo hayo, Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango akimkabidhi zawadi ya mchoro wa Mlima Kilimanjaro Naibu Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Maendeleo ya Ufaransa (AFD) Bi. Marie-Hellen Loison mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao Paris, Ufaransa.

No comments