JOB NDUGAI; KAMA UNAPINGA TOZO TUPE NJIA
Spika wa Bunge, Job Ndugai, amepigilia msumari kwenye tozo ya miamala katika simu kwa kudai bunge ndio limepitisha na wale ambao wanapinga wanatakiwa kutoa mawazo mbadala nini kifanyike huku akisisitiza lengo ni ifikapo 2025 Tanzania liwe Taifa tofauti katika suala la Maendeleo.
Hatua hiyo imekuja kufuatia baadhi ya wananchi kulalamika kwamba kumekuwa na tozo kubwa katika miamala ya simu.
Akizungumza leo, Julai 23, 2021, katika kikao kazi kilichoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka, ambapo amesema wao kama bunge ndio wameamua kuwe na tozo katika miamala ya simu kwa sababu fedha zitakakazopatikana zitaenda katika mfuko Maalum ambao utawasaidia wananchi.
"Tumepitisha sisi, tukatunga sheria sisi, tunataka kuliona hilo, sasa wewe ambaye unapinga tupe njia mbadala tutapata wapi fedha, tunafikaje 2025, kwa hiyo maamuzi ni hayo tumeyafanya, kwa nia njema kabisa kwamba 2025 tuwe tumetoka, tuwe ni taifa la Tanzania ambalo ni tofauti... CCM hoyee, nimemaliza,"amesema Spika Ndugai.
Aidha, akizungumzia kuhusu mkoa wa Dodoma amewataka watendaji wa mkoa huo kujitathimini katika utekelezaji wa majukumu yao kwani serikali imekuwa ikitimiza wajibu wake kwa kuleta fedha kwa wakati lakini tatizo lipo kwa watendaji.
"Hapa nitolee mfano mkuu wa mkoa wa Antony Mtaka aliyetoka Simuyu kule alifanya kazi nzuri, hivyo hapa akishindwa kufanya vizuri tujue kabisa tatizo lipo kwetu," amesema Ndugai.
Kwa upande wake mkoa wa Dodoma, Mtaka amebainisha vipaumbele vinne ambavyo atavisimamia katika mkoa wa Dodoma.
Mtaka amevitaja vipaumbel hivyo kuwa ni pamoja na elimu, migigoro ya ardhi, kilimo na ufugaji wenye tija na huduma bora za sekta za afya huku akitangaza alizeti kuwa zao la biashara katika mkoa huo.

Post a Comment