JIANG AITAKA CANADA KUFANYA UCHUNGUZI JUU YA MABAKI 751

Jiang Duan, afisa mwandamizi katika misheni ya China kwa UN huko Geneva, amesema Canada inatakiwa ijitoe kwa moyo mmoja baada ya mabaki ya zaidi ya watoto wa asili 1,000 kupatikana katika shule za zamani za makazi nchini humo.

Duan ametoa wito kwa Canada kufanya uchunguzi kamili na kwa umakini kwa watu wanaohusika na kushughulikia ubaguzi wake wa kimfumo na uhalifu wa chuki.

Mabaki ya miili ya watoto 751 yalipatikana kwenye makaburi ambayo hayakujulikana katika bustani ya
Shule ya Bweni ya Marieval huko Saskatchewan, Canada.

Cadmus Delorme, Mkuu wa Wazawa wa Taifa la Kwanza wa Mkoa wa Cowessess ambapo makaburi yalipatikana, alisema katika mkutano na waandishi wa habari kwamba makaburi 751 ambayo hayamo kwenye kumbukumbu rasmi hadi sasa yamegunduliwa kama matokeo ya kazi iliyotekelezwa tangu mwanzoni mwa mwezi huu.

No comments