UCHAGUZI WA MKE BORA



Maisha....
Unaweza ukawa una date msichana mrembo, nadhifu, anapendeza machoni mwa kila mtu.

Lakini bado akawa hana sifa za kufanywa kuwa mke.

Suala la ndoa huwa halihusiani na urembo wa mwanamke unayetaka kumuoa.

Bali kwa asilimia kubwa  linahusiana na aina ya mwanamke ambaye unahitaji kumuoa kwa kutazama yafuatayo:

i: Akili yake, misimamo yake, uvumilivu wake, kujitambua kwake.
Sababu mwanamke aliyekosa sifa hizo, huwa ni tatizo kubwa sana ndani ya ndoa.

ii: Tabia zake, imani yake, upendo wake kwako na kwa ndugu zako.

Unahitaji kuoa mwanamke mwenye tabia njema, hofu ya Mungu, na mwenye kukupenda wewe na ndugu zako.

iii: Uwezo wake wa kusimamia nafasi yake kama msaidizi wako na majukumu yake ndani ya nyumba.

 Sababu ni kero kuwa na mwanamke ambaye hajitambui, Hajui majukumu yake. Pata picha unakuwa na mke ambaye hajui kupika wala kufanya usafi.

v: Ili uweze kuifurahia ndoa yako, ni vyema kujua kabisa kama upo na mtu sahihi kwako ambaye atakupa amani ya moyo, na tulizo la akili yako. Au Ndo upo na kivuruge ambaye atakujaza stress za mapenzi kila kukicha.

v: Yote juu ya yote, unahitaji maendeleo hivyo ni vyema kujua support yake ipoje, anakupa hamasa kiasi gani, au ndio chanzo cha kukuvunja moyo? Kukufilisi?
 Pamoja na kukuongeza stress za majukumu yasiyo ya lazima..

Kuwa smart leo kwenye uchaguzi wa mwanamke wa kuoa, ili kuepusha stress zitakazofanya uichukue ndoa yako kwa hapo baadae.

No comments