HEMED ABDULLAH KUFUNGA RASMI MAONESHO YA 45 YA (DITF)

Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Hemed Abdullah kufunga rasmi maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF).

Hayo yamesemwa Jana na Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe alipokutana na waandishi wa habari kuzungumza kuhusu ufungaji wa Maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yaliyoanza tarehe 28 Juni, 2021 ambayo yanatarajiwa kumalizika tarehe 13 Julai, 2021 katika Uwanja wa Maonesho wa Mwl. J.K. Nyerere, Barabara ya Kilwa, Dar es Salaam.

Mhe. Kigahe amesema kuwa Maonesho ya mwaka huu yamekuwa na jumla ya washiriki 3,002 kutoka ndani na nje ya Tanzania. Washiriki hao wanatoka kwenye Wizara, Taasisi, Makampuni, Wafanyabiashara, Wajasiriamali wadogo na Watoa Huduma mbalimbali na nchi zipatazo 16 zimewakilishwa na jumla ya makampuni 76 ambayo yameonesha teknolojia, huduma na bidhaa mbalimbali kwa ajili ya kupata wabia, mawakala na wasambazaji wa bidhaa na huduma zao.

Aidha Mhe. Kigahe amesema kuwa tangu kuanza kwa Maonesho hayo tarehe 28 Juni, 2021 jumla ya Wageni 121 ambao ni Viongozi wa Chama na Serikali, Mabalozi, Wakuu wa Taasisi za Umma na Binafsi na Mashirika ya Kimataifa na Viongozi wa Dini wametembelea Maonesho haya na kujionea bidhaa na huduma zinazozalishwa na viwanda vikubwa na vidogo.

Mhe. Kigahe amesema kuwa Kauli Mbiu ya Maonesho ya mwaka huu ilikuwa ni “Uchumi wa Viwanda kwa Ajira na Biashara Endelevu” ambapo Kauli mbiu hiyo ililelenga kutambua mchango wa Sekta ya Viwanda katika kuongeza ajira na uzalishaji wa Mazao ya Kilimo, Madini, Uvuvi, Mifugo, Misitu na kuchochea biashara kwa maendeleo ya uchumi wetu.

Mhe. Kigahe ameeleza shughuli mbalimbali zilizofanyika wakati wote wa maonesho ni pamoja na, Mikutano ya Biashara (Business to Business - B2B) kwa Njia ya Mtandao na ilijikita kwenye bidhaa za Nyama, Matunda na Mbogamboga, Nafaka, Mikunde, Mahindi, Samaki, Viungo, Mihogo, Kahawa, Korosho, Chai, Ufuta na Teknolojia ambayo inaratibiwa na TanTrade kwa kushirikiana na Ofisi za Balozi za Tanzania zilizopo Nje ya Nchi, Uzinduzi wa Tela la Trekta lililotengenezwa na Kampuni ya Kilimanjaro Machine Tools (KMTC) iliyo chini ya Shirika la Taifa la Maendeleo

No comments