• HOME
  • BREAKING NEWS
  • TAMTHILIA
  • MICHEZO
  • MATANGAZO
  • CONTACT US

BINAGO BLOG

  • Home
  • Home / Habari / CHUO CHA (CBE) CHATAKIWA KUTOA WAHITIMU WENYE UJUZI

    CHUO CHA (CBE) CHATAKIWA KUTOA WAHITIMU WENYE UJUZI

    Bisaya Raphael July 13, 2021 Habari
    Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb) ameiagiza Bodi ya Uongozi wa Chuo cha Biashara (CBE) kusimamia Chuo katika utoaji wa huduma bora katika jamii kwa kutoa elimu ya biashara kwa wajasiriamali, kutoa wahitimu wenye ujuzi kulingana na uhitaji wa soko na kutoa mafunzo na kutoa ushauri wa kitaalamu kwa Maafisa biashara.

    Prof. Mkumbo ameyasema hayo Julai 12, 2021 katika hafla fupi ya uzinduzi wa Bodi ya Uongozi wa Chuo cha Biashara (CBE) iliyofanyika katika Chuo hicho Dar es salaam na kuhudhuliwa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe, Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Bw. Doto James, Mkuu wa Chuo cha CBE Prof. Emanuel Mjema na Uongozi wa Wanafunzi wa Chuo hicho.

    Prof. Mkumbo aliitaka Bodi hiyo kuandaa mpango wa upimaji wa matokeo kwa kuzingatia maeneo matatu ya majukumu ya Bodi ambayo ni kutoa ushauri katika maeneo yenye tija kwa Taasisi ndani na nje ya vikao vya Bodi, kuwa mtunza nidhamu wa Mkuu wa Taasisi na Menejimenti ya Taasisi kwa niaba ya mmiliki wa Chuo ambayo ni Serikali na kutoa utatuzi pale Taasisi inapokuwa inakabiliwa na changamoto za kimenejimenti.

    Aidha, Prof. Mkumbo aliiasa Bodi kutekeleza majukumu yake kikamilifu kwa kuzingatia uelewa mzuri wa maana, malengo, na majukumu ya Taasisi, sheria na kanuni zinazoendesha Taasisi, Kuwa na viwango na vigezo vya kupima utendaji wa Menejimenti, kuelewa majukumu yake sawa sawa na wajumbe kujiepusha na kufanya kazi za Menejimenti, Ushirikiano, kuthaminiani, kusikilizana na upendo na Falsafa ya utendaji wa Bodi.

    Nae, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe aliutaka uongozi wa chuo kutoa elimu, ujuzi na kuwajengea wanafunzi uelewa na uwezo wa kuthubutu wa kufanya jambo wanalodhani ni muhimu ili wanapohitimu waamue kutafuta ajira au kujiajiri ili kuondokana na dhana ya kuwa Serikali haiwasaidii.

    Kwa Upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Uongozi ya Chuo cha Elimu ya Biashara Prof. Eliuther Mwageni alitoa shukurani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa imani kubwa ya kumteua kuwa Mwenyekiti wa Bodi huku akiahidi kushirikiana na wajumbe wa bodi kutekeleza majukumu yao kwa weledi na uadilifu.

    Related Posts

    Habari

    Post a Comment

    No comments

    Subscribe to: Post Comments ( Atom )

    KWA SHEREHE NA SEMINA KARIBU UKUMBI WA LAKE TANGANYIKA, NZEGA-TABORA

    FOOTBALL STORIES

    Follow us

    • Like on Facebook
    • Follow on Twitter
    • Follow on Instagram
    • Subscribe on Youtube

    Popular Posts

    • kusuka na unyoaji katika Biblia
      kusuka na unyoaji katika Biblia
       KAMA MUNGU ALIVYOKWISHA KUWAONYA WANAWAKE ! NDIVYO ALIVYOKWISHA KUWAONYA WANAUME PIA. BWANA YESU asifiwe!😅 Maranatha!😅🙏🏻 N...
    • Je kutoa Mahari ni sawa ktk biblia?
      Je kutoa Mahari ni sawa ktk biblia?
      *https://youtu.be/-P4s8sVq31o* 🤔🤔🤔🤔🤔 *JE NI HALALI KWA MKRISTO KULIPA MAHARI ILI AOE?????* 🤔🤔🤔🤔🤔 . . . Hebu tutazame k...
    • HII NDIO MISINGI YA KANISA LA WASABATO DUNIANI
      HII NDIO MISINGI YA KANISA LA WASABATO DUNIANI
      KANISA LA #SDA LINA MISINGI 28 AMBAYO NI 1.Neno la Mungu 2.Utatu mtakatifu 3.Mungu baba 4.Mungu mwana 5.Roho mtakatifu 6.Uumbaji...

    Labels

    Habari MICHEZO Live injili Tamthilia Kesha la Asubuhi BREAKING NEWS magazeti Matangazo Covid19 Mastaa Viongozi today's quote Lesoni leo Wimbo wa Leo barikiwa Je Wajua? KULFI Bongo Movies Stories TETESI ZA USAJILI

    Facebook

    Created By SoraTemplates | Distributed By Gooyaabi Templates